Biblia inasema nini kuhusu kuingia miungu kupumzika – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuingia miungu kupumzika

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuingia miungu kupumzika

Mathayo 11 : 28
28 Njooni kwangu, ninyi nyote msumbukao na wenye kulemewa na mizigo, nami nitawapumzisha.

Waraka kwa Waebrania 4 : 1 – 16
1 ⑬ Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.
2 Maana ni kweli, sisi nasi tumehubiriwa Habari Njema vile vile kama hao. Lakini neno lile lililosikiwa halikuwafaa hao, kwa sababu halikuchanganyika na imani ndani yao waliosikia.
3 ⑭ Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia pumzikoni mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.
4 ⑮ Kwa maana ameinena siku ya saba mahali fulani hivi, Mungu alistarehe siku ya saba, akaziacha kazi zake zote;
5 ⑯ na tena kunena hapa napo, Hawataingia pumzikoni mwangu.
6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,
7 ⑰ aweka tena siku fulani, akisema katika Daudi baada ya muda mwingi namna hii, Leo, kama ilivyonenwa tangu zamani, Leo, kama mkisikia sauti yake, Msifanye mioyo yenu migumu.
8 ⑱ Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.
9 Basi, limesalia pumziko la sabato kwa watu wa Mungu.
10 ⑲ Kwa maana yeye aliyeingia katika pumziko lake amepumzika mwenyewe katika kazi yake, kama vile Mungu alivyopumzika katika kazi zake.
11 Basi, na tufanye bidii kuingia katika pumziko lile, ili kwamba mtu yeyote asije akaanguka kwa mfano uo huo wa kuasi.
12 ⑳ Maana neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena ni jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.
13 Wala hakuna kiumbe kisichokuwa wazi mbele zake, maana vitu vyote ni tupu na kuwekwa wazi machoni pake yeye ambaye tunapaswa kuwajibika kwake.
14 Basi, iwapo tunaye kuhani mkuu aliyeingia katika mbingu, Yesu, Mwana wa Mungu, na tuyashike sana maungamo yetu.
15 Kwa kuwa hamna kuhani mkuu asiyeweza kuchukuana nasi katika mambo yetu ya udhaifu; bali yeye alijaribiwa kama sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi.
16 Basi na tukikaribie kiti cha neema kwa ujasiri, ili tupewe rehema, na kupata neema ya kutusaidia wakati wa mahitaji.

Waraka kwa Waebrania 4 : 1
1 ⑬ Basi, ikiwa ingalipo ahadi ya kuingia katika pumziko lake, na tuogope, mmoja wenu asije akaonekana ameikosa.

Zaburi 95 : 7 – 11
7 ④ Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
8 ⑤ Msifanye mioyo yenu kuwa migumu; Kama ilivyokuwa huko Meriba Kama siku ile katika Masa jangwani.
9 Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10 ⑥ Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile, Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka, Na wanaopuuza njia zangu.
11 ⑦ Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu Hawataingia katika pumziko langu.

Waraka kwa Waebrania 3 : 19
19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao.

Waraka kwa Waebrania 4 : 8
8 ⑱ Maana kama Yoshua angaliwapa pumziko, asingaliinena siku nyingine baadaye.

Zaburi 95 : 1 – 11
1 Njoni, tumwimbie BWANA, Tumfanyie shangwe mwamba wa wokovu wetu.
2 Tuje mbele zake kwa shukrani, Tumfanyie shangwe kwa zaburi.
3 Kwa kuwa BWANA ni Mungu mkuu, Na Mfalme mkuu juu ya miungu yote.
4 Mkononi mwake zimo bonde za dunia, Hata vilele vya milima ni vyake.
5 Bahari ni yake, ndiye aliyeifanya, Na mikono yake iliumba nchi kavu.
6 ③ Njoni, tuabudu, tusujudu, Tupige magoti mbele za BWANA aliyetuumba.
7 ④ Kwa maana ndiye Mungu wetu, Na sisi tu watu wa malisho yake, Na kondoo za mkono wake. Ingekuwa heri leo msikie sauti yake!
8 ⑤ Msifanye mioyo yenu kuwa migumu; Kama ilivyokuwa huko Meriba Kama siku ile katika Masa jangwani.
9 Hapo waliponijaribu baba zenu, Wakanipima, wakayaona matendo yangu.
10 ⑥ Miaka arubaini nilichukizwa na kizazi kile, Nikasema, Hawa ni watu wenye mioyo inayopotoka, Na wanaopuuza njia zangu.
11 ⑦ Ndipo Nikaapa kwa hasira yangu Hawataingia katika pumziko langu.

Waraka kwa Waebrania 4 : 6
6 Basi, kwa kuwa neno hili limebaki kwamba wako watu watakaoingia humo, na wale waliohubiriwa habari ile zamani walikosa kuingia kwa sababu ya kuasi kwao,

Waraka kwa Waebrania 3 : 1 – 19
1 Kwa hiyo, ndugu watakatifu, wenye kuushiriki mwito wa mbinguni, mtafakarini sana Mtume na Kuhani Mkuu wa maungamo yetu, Yesu,
2 aliyekuwa mwaminifu kwake yeye aliyemweka, kama Musa naye alivyokuwa, katika nyumba yote ya Mungu.
3 Kwa maana huyo amehesabiwa kuwa amestahili utukufu zaidi kuliko Musa, kama vile yeye aitengenezaye nyumba alivyo na heshima zaidi ya hiyo nyumba.
4 Maana kila nyumba imetengenezwa na mtu; ila yeye aliyevitengeneza vitu vyote ni Mungu.
5 ① Na Musa kweli alikuwa mwaminifu katika nyumba yote ya Mungu kama mtumishi, awe ushuhuda wa mambo yatakayonenwa baadaye;
6 ② bali Kristo, kama mwana, juu ya nyumba ya Mungu; ambaye nyumba yake ni sisi, kama tukishikamana sana na ujasiri wetu na fahari ya tumaini letu mpaka mwisho.
7 ③ Kwa hiyo, kama anenavyo Roho Mtakatifu, Leo, kama mkisikia sauti yake,
8 ④ Msifanye mioyo yenu kuwa migumu, Kama wakati wa kuasi, Siku ya kujaribiwa katika jangwa,
9 Hapo baba zenu waliponijaribu, wakanipima, Wakaona matendo yangu miaka arubaini.
10 Kwa hiyo nilichukizwa na kizazi hiki, Nikasema, Sikuzote ni watu waliopotoka mioyo hawa; Hawakuzijua njia zangu;
11 ⑤ Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia rahani mwangu.
12 Hadharini, ndugu zangu, usiwepo katika mmoja wenu moyo mbovu wa kutoamini, ujitengao na Mungu aliye hai.
13 ⑥ Lakini mwonyane kila siku, maadamu inaitwa leo; ili mmoja wenu asifanywe mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14 ⑦ Kwa maana tumekuwa washirika wa Kristo, kama tukishikamana na mwanzo wa uthabiti wetu kwa nguvu mpaka mwisho;
15 ⑧ kama inenwavyo, Leo, kama mkisikia sauti yake, Msifanye mioyo yenu kuwa migumu, Kama wakati wa kuasi.
16 ⑩ Maana ni akina nani walioasi, waliposikia? Si wale wote waliotoka Misri wakiongozwa na Musa?
17 ⑪ Tena ni akina nani aliochukizwa nao miaka arubaini? Si wale waliokosa, ambao mizoga yao ilianguka katika jangwa?
18 ⑫ Tena ni akina nani aliowaapia ya kwamba hawataingia katika pumziko lake, ila wale walioasi?
19 Basi twaona ya kuwa hawakuweza kuingia kwa sababu ya kutoamini kwao.

Waraka kwa Waebrania 4 : 3
3 ⑭ Maana sisi tulioamini tunaingia katika pumziko lile; kama vile alivyosema, Kama nilivyoapa kwa hasira yangu, Hawataingia pumzikoni mwangu: ijapokuwa zile kazi zilimalizika tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu.

Kumbukumbu la Torati 28 : 1 – 68
1 ⑳ Itakuwa utakaposikia sauti ya BWANA, Mungu wako, kwa bidii, kutunza kuyafanya maagizo yake yote nikuagizayo leo, ndipo BWANA, Mungu wako, atakapokutukuza juu ya mataifa yote ya duniani;
2 na baraka hizi zote zitakujilia na kukupata usikiapo sauti ya BWANA, Mungu wako.
3 Utabarikiwa mjini, utabarikiwa na mashambani.
4 Utabarikiwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, kuongezeka kwa ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
5 Litabarikiwa kapu lako, na chombo chako cha kukandia unga.
6 Utabarikiwa uingiapo, utabarikiwa na utokapo.
7 BWANA atawafanya adui zako wainukao juu yako kupigwa mbele yako; watakutokea kwa njia moja, lakini watakimbia mbele yako kwa njia saba.
8 BWANA ataiamuru baraka ije juu yako katika ghala zako, na mambo yote utakayotia mkono wako; naye atakubarikia katika nchi akupayo BWANA, Mungu wako.
9 BWANA atakuweka uwe taifa takatifu kwake, kama alivyokuapia; utakaposhika maagizo ya BWANA, Mungu wako, na kutembea katika njia zake.
10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.
11 BWANA atakufanya uwe na wingi wa uheri, katika uzao wa tumbo lako, na uzao wa wanyama wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako, katika nchi BWANA aliyowaapia baba zako kwamba atakupa.
12 Atakufunulia BWANA hazina yake nzuri, nayo ni mbingu, kwa kutoa mvua ya nchi yako kwa wakati wake, na kwa kubarikia kazi yote ya mkono wako; nawe utakopesha mataifa mengi, wala hutakopa wewe.
13 BWANA atakufanya kuwa kichwa, wala si mkia; nawe utakuwa juu tu, wala huwi chini; utakapoyasikiza maagizo ya BWANA, Mungu wako, nikuagizayo hivi leo, kuyaangalia na kufanya;
14 msipokengeuka katika maneno niwaamuruyo leo kwa lolote, kwenda mkono wa kulia wala wa kushoto, kwa kuifuata miungu mingine na kuitumikia.
15 Lakini itakuwa usipotaka kuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, usiyaangalie kufanya maagizo yake yote na amri zake, nikuagizazo hivi leo, ndipo zitakapokujia laana hizi zote na kukupata.
16 Utalaaniwa mjini, utalaaniwa na mashambani.
17 Litalaaniwa kapu lako na chombo chako cha kukandia.
18 Utalaaniwa uzao wa tumbo lako, na uzao wa nchi yako, kuongezeka kwa ng’ombe wako, na wadogo wa kondoo wako.
19 Utalaaniwa uingiapo, utalaaniwa na utokapo,
20 BWANA atakuletea laana na mashaka, na kukemewa, katika yote utakayotia mkono wako kuyafanya, hata uangamie na kupotea kwa upesi; kwa ule uovu wa matendo yako, uliyoniacha kwayo.
21 BWANA atakuambatanisha na tauni, hata atakapokwisha kukuondoa katika nchi uingiayo kwa kuimiliki.
22 BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
23 Na mbingu zako zilizo juu ya kichwa chako zitakuwa shaba, na nchi iliyo chini yako itakuwa chuma.
24 BWANA atafanya mvua ya nchi yako iwe vumbi na mchanga; itakujilia juu yako kutoka mbinguni hata uangamie.
25 BWANA atakufanya upigwe mbele ya adui zako; utawatokea juu yao kwa njia moja, lakini utakimbia mbele yao kwa njia saba; nawe utatupwa huku na huko katika falme zote za duniani.
26 Na mzoga wako utakuwa chakula cha ndege wote wa angani, na wanyama wote wa duniani, pasiwe na mtu wa kuwafukuza.
27 BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
28 BWANA atakupiga kwa wazimu, na kwa upofu, na kwa bumbuazi la moyoni;
29 utakwenda kwa kupapasapapasa mchana, kama apapasavyo kipofu gizani, wala hufanikiwi katika njia zako; nawe sikuzote utaonewa na kutekwa nyara, wala hapatakuwa na mtu wa kukuokoa.
30 Utaposa mke na mume mwingine atalala naye; utajenga nyumba usiikae; utapanda mizabibu usitumie matunda yake.
31 Ng’ombe wako atachinjwa mbele ya macho yako, usile nyama yake; utanyang’anywa punda wako mbele ya uso wako kwa jeuri, usirudishiwe; kondoo wako watapewa adui zako, usipate mtu wa kukuokoa.
32 Wanao na binti zako litapewa taifa lingine, na macho yako yataangalia, na kuzimia kwa kuwatamani mchana kutwa; wala hapatakuwa na kitu katika uwezo wa mkono wako.
33 Matunda ya nchi yako, na taabu yako yote, vitaliwa na taifa usilolijua; utaonewa tu, na kupondwa chini daima;
34 hata uwe mwenye wazimu kwa yaonwayo na macho yako, utakayoyaona.
35 BWANA atakupiga magoti na miguu kwa jipu lililo zito, usilopata kupozwa, tokea wayo wa mguu mpaka utosi wa kichwa.
36 BWANA atakupeleka wewe, na mfalme wako utakayemweka juu yako, kwa taifa usilolijua wewe wala baba zako; nawe huko utatumikia miungu mingine ya miti na mawe.
37 Nawe utakuwa ushangao, na mithali, na dharau, kati ya mataifa yote huko atakakokuongoza BWANA.
38 Mbegu nyingi utazichukua nje shambani, lakini utavuna haba, kwa kuwa nzige watazila.
39 Utapanda mizabibu na kuitengeza, wala hutakunywa katika divai yake, wala kuichuma kwani italiwa na mabuu.
40 Utakuwa na mizeituni katika mipaka yako yote usijipake mafuta yake; kwa kuwa mzeituni wako utapukutika.
41 Utazaa wana na binti, lakini hawatakuwa wako wewe; kwa sababu watakwenda utumwani.
42 Miti yako yote, na mazao ya nchi yako, nzige watakuwa nayo.
43 Mgeni aliye kati yako atazidi kupaa juu yako; nawe utazidi kushuka chini.
44 Yeye atakukopesha, wala wewe usimkopeshe; yeye atakuwa ni kichwa, wewe utakuwa mkia.
45 Na laana hizi zote zitakujilia juu yako, zitakuandama na kukupata, hata uangamizwe, kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako, kushika maagizo yake na amri zake alizokuagiza;
46 nazo zitakuwa juu yako kwa ishara na ajabu, na juu ya uzao wako milele;
47 ① kwa kuwa hukumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa furaha na moyo wa kushukuru, kwa ajili ya ule wingi wa vitu vyote;
48 ② kwa hiyo utawatumikia adui zako atakaowaleta BWANA juu yako, kwa njaa, na kwa kiu, na kwa uchi, na kwa uhitaji wa vitu vyote; naye atakuvika kongwa la chuma shingoni mwako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
49 ③ BWANA atakuletea taifa juu yako kutoka mbali, kutoka ncha ya dunia, kama arukavyo tai; taifa usiloufahamu ulimi wake;
50 ④ taifa lenye uso mkali, ambalo haliangalii uso wa mzee, wala halipendelei kijana;
51 ⑤ naye atakula uzao wa ng’ombe wako wa mifugo, na uzao wa nchi yako mpaka utakapokwisha kuangamizwa; wala hatakuachia nafaka, wala divai, wala mafuta, wala kuongezeka kwa ng’ombe wako, wala wana-kondoo wako, hata atakapokwisha kukuangamiza.
52 ⑥ Naye atakuhusuru katika malango yako yote, hata kuta zako ndefu, zenye maboma, ulizokuwa ukiziamini, zishuke, katika nchi yako yote kila upande; naye atakuhusuru katika malango yako yote kila upande, katika nchi yako yote aliyokupa BWANA, Mungu wako.
53 ⑦ Nawe utakula uzao wa tumbo lako mwenyewe, nyama ya wana wako na binti zako aliokupa BWANA, Mungu wako; katika mazingirwa na katika mkazo utakaokazwa na adui zako.
54 Mtu mume kati yenu aliye mwororo na laini sana, jicho lake litakuwa ovu juu ya nduguye, na juu ya mke wa kifuani mwake, na juu ya masalio ya wanawe waliosalia naye;
55 hata asitake wao mmojawapo apewe katika nyama ya wanawe atakaowala, kwa kuwa hana kitu kilichomsalia kwake; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako yote.
56 Mwanamke kati yenu aliye mwororo na laini, ambaye hangehatarisha kuweka wayo wa mguu wake nchi kwa umalidadi na ulaini, jicho lake huyu litakuwa ovu juu ya mume wa kifuani mwake, na juu ya mwanawe, na juu ya binti yake,
57 ⑧ na juu ya mchanga wake atokaye katikati ya miguu yake, na juu ya wanawe atakaowazaa; kwa kuwa atawala kwa siri, kwa uhitaji wa vitu vyote; katika mazingirwa na mkazo utakaokazwa na adui yako katika malango yako.
58 ⑩ Kama hutaki kutunza kufanya maneno yote ya torati hii yaliyoandikwa katika kitabu hiki, upate kulicha jina hili la fahari na utisho, BWANA, MUNGU WAKO;
59 ⑪ ndipo atakapofanya BWANA mapigo yako yawe ya ajabu, na mapigo ya uzao wako, mapigo makubwa kwa kweli, ya kudumu sana, na magonjwa mazito ya kudumu sana.
60 Naye atakurejezea maradhi yote ya Misri juu yako uliyokuwa ukiyaogopa, nayo yataambatana nawe.
61 Tena kila ugonjwa, na kila pigo yasiyoandikwa katika kitabu cha Torati hii, atakutia nayo BWANA juu yako, hata utakapokwisha kuangamizwa.
62 ⑫ Nanyi mtasalia wachache kwa hesabu, ninyi mliokuwa mfano wa nyota za mbinguni kwa wingi; kwa kuwa hukuisikiza sauti ya BWANA, Mungu wako.
63 ⑬ Tena itakuwa, kama vile alivyokuwa akifurahi BWANA juu yenu kwa kuwatendea mema na kuwafanya kuwa wengi, ndivyo atakavyofurahi BWANA juu yenu kwa kuwapoteza na kuwaangamiza; nanyi mtanyakuliwa katika hiyo nchi mwingiayo kuimiliki.
64 ⑭ BWANA atakutawanya katika mataifa yote, tokea ncha hii ya dunia hata ncha hii ya dunia; nawe huko utatumikia miungu mingine usiyoijua wewe wala baba zako, nayo ni miti na mawe.
65 ⑮ Wala katika mataifa hayo hutapata raha iwayo yote, wala hutakuwa na kituo cha wayo wa mguu wako; lakini BWANA atakupa huko moyo wa kutetema, na macho ya kuzimia, na roho ya kudhoofika;
66 na uzima wako utakuwa na wasiwasi mbele yako; nawe utakuwa na woga usiku na mchana, wala hutaamini kamwe maisha yako;
67 ⑯ asubuhi utasema, Laiti ingekuwa jioni! Na jioni utasema, Laiti ingekuwa asubuhi! Kwa kicho cha moyo wako utakavyokucha, na kuona kwa macho yako utakavyoona.
68 ⑰ BWANA atakurudisha tena Misri kwa merikebu, kwa njia ambayo nilikuambia, Hutaiona tena popote; nanyi huko mtajiuza nafsi zenu kwa adui zenu kuwa watumwa na wajakazi, wala hapana atakayewanunua.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *