Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuhubiri
Mhubiri 1 : 1
1 Maneno ya Mhubiri[1] mwana wa Daudi, mfalme katika Yerusalemu
Mhubiri 1 : 12
12 Mimi, Mhubiri, nilikuwa Mfalme wa Israeli katika Yerusalemu.
2 Petro 2 : 5
5 wala hakuuachilia ulimwengu wa kale, bali alimhifadhi Nuhu, mjumbe wa haki, na watu wengine saba, hapo alipoleta Gharika juu ya ulimwengu wa wasiomcha Mungu;
Mathayo 5 : 1
1 Naye alipowaona makundi ya watu, alipanda mlimani; na alipokwisha kuketi, wanafunzi wake walimjia;
Luka 4 : 20
20 Akakifunga kitabu, akamrudishia mtumishi, akaketi; na watu wote waliokuwamo katika sinagogi wakamkazia macho.
Luka 5 : 3
3 Akaingia katika mashua moja, ndiyo yake Simoni, akamtaka aipeleke mbali kidogo na pwani. Akaketi, akawafundisha makutano akiwa katika mashua.
Kutoka 4 : 12
12 Basi sasa, nenda, nami nitakuwa pamoja na kinywa chako, na kukufundisha utakalolinena.
Mathayo 3 : 2
2 ④ Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Marko 1 : 4
4 Yohana alitokea, akibatiza nyikani, na kuuhubiri ubatizo wa toba liletalo ondoleo la dhambi.
Marko 1 : 15
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Luka 3 : 3
3 Akafika katika nchi yote iliyo karibu na Yordani, akihubiri ubatizo wa toba iletayo ondoleo la dhambi,
Mathayo 4 : 17
17 Tokea wakati huo Yesu alianza kuhubiri, na kusema, Tubuni; kwa maana ufalme wa mbinguni umekaribia.
Marko 1 : 15
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Marko 6 : 12
12 Wakatoka, wakahubiri kwamba watu watubu.
Marko 1 : 15
15 akisema, Wakati umetimia, na ufalme wa Mungu umekaribia; tubuni, na kuiamini Injili.
Marko 2 : 2
2 Wakakusanyika watu wengi, isibaki nafasi hata mlangoni; akawa akisema nao neno lake.
Luka 8 : 1
1 ⑰ Ikawa baada ya hayo alikuwa akizungukazunguka katika miji na vijiji akihubiri na kuitangaza Habari Njema ya ufalme wa Mungu; na wale Kumi na Wawili walikuwa pamoja naye,
Leave a Reply