Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuheshimu wengine
Mathayo 5 : 43 – 48
43 Mmesikia kwamba imenenwa, Umpende jirani yako, na, Umchukie adui yako;
44 lakini mimi nawaambia, Wapendeni adui zenu, waombeeni wanaowaudhi,
45 ili mpate kuwa wana wa Baba yenu aliye mbinguni; maana yeye huwaangazia jua lake waovu na wema, huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki.
46 Maana mkiwapenda wanaowapenda ninyi mnapata thawabu gani? Hata watoza ushuru, je! Nao hawafanyi yayo hayo?
47 Tena mkiwaamkia ndugu zenu tu, mnatenda tendo gani la ziada? Hata watu wa mataifa, je! Nao hawafanyi sawa na hayo?
48 Basi ninyi iweni wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.
Warumi 12 : 10
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
Wakolosai 3 : 20
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
Waefeso 6 : 1 – 4
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 ① Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
4 ② Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Luka 6 : 30 – 36
30 Mpe kila akuombaye, na akunyang’anyaye vitu vyako, usitake akurudishie.
31 Na kama mnavyotaka watu wawatendee ninyi, watendeeni vivyo hivyo.
32 Maana mkiwapenda wale wawapendao ninyi, mwaonesha fadhili gani? Kwa kuwa hata wenye dhambi huwapenda wale wawapendao.
33 Nanyi mkiwatendea mema wale wawatendeao mema, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi hufanya vivyo hivyo.
34 Na mkiwakopesha watu huku mkitumaini kupata kitu kwao, mwaonesha fadhili gani? Hata wenye dhambi huwakopesha wenye dhambi, ili warudishiwe vile vile.
35 Bali wapendeni adui zenu, tendeni mema, na kukopesha msitumaini kupata malipo, na thawabu yenu itakuwa nyingi; nanyi mtakuwa wana wa Aliye Juu, kwa kuwa yeye ni mwema kwa wasiomshukuru, na waovu.
36 Basi, iweni na huruma, kama Baba yenu alivyo na huruma.
Mithali 1 : 8
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
Warumi 13 : 7
7 ② Wapeni wote haki zao; mtu wa kodi, kodi; mtu wa ushuru, ushuru; astahiliye hofu, hofu; astahiliye heshima, heshima.
1 Wakorintho 4 : 6
6 Basi ndugu, mambo hayo nimeyafanya kuwa mfano wa mimi na Apolo kwa ajili yenu, ili kwamba kwa mfano wetu mpate kujifunza kutokupita yale yaliyoandikwa; ili mmoja wenu asijivune kwa ajili ya huyu, kinyume cha mwenziwe.
Mithali 1 : 8 – 9
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
9 Kwa maana hayo yatakuwa kilemba cha neema kichwani pako, Na mikufu shingoni mwako.
Mambo ya Walawi 19 : 15
15 ⑲ Msitende yasiyo haki katika hukumu, usimpendelee mtu maskini, wala kumstahi mwenye nguvu; bali utamhukumu jirani yako kwa haki.
Leave a Reply