Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuheshimu wazazi
Kutoka 20 : 12
12 Waheshimu baba yako na mama yako; siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na BWANA, Mungu wako.
Wakolosai 3 : 20
20 Ninyi watoto, watiini wazazi wenu katika mambo yote; maana jambo hili lapendeza katika Bwana.
Waefeso 6 : 1 โ 4
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
2 โ Waheshimu baba yako na mama yako; hii ndiyo amri ya kwanza yenye ahadi,
3 Upate heri na kuishi siku nyingi katika dunia.
4 โก Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Waefeso 6 : 1
1 Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo haki.
Mithali 1 : 8
8 Mwanangu, yasikilize mafundisho ya baba yako, Wala usiiache sheria ya mama yako,
Kumbukumbu la Torati 21 : 18 โ 21
18 โซ Mtu akiwa na mwana mkaidi, mshupavu, asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu hawasikizi,
19 ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa mji wake, katika lango la mahali pake;
20 wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana wetu ni mkaidi, mshupavu, hasikizi sauti yetu; ni mwasherati, tena ni mlevi.
21 โฌ Wanaume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe; ndivyo utakavyoondoa uovu katikati yako; na Israeli wote watasikia na kuogopa.
Kumbukumbu la Torati 4 : 10
10 โช siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.
Kutoka 21 : 17
17 Yeye amwapizaye baba yake au mama yake, sharti atauawa.
Mithali 22 : 6
6 Mlee mtoto katika njia impasayo, Naye hataiacha, hata atakapokuwa mzee.
Mithali 13 : 24
24 Yeye asiyetumia fimbo yake humchukia mwanawe; Bali yeye ampendaye humrudi mapema.
Mithali 29 : 15
15 Fimbo na maonyo hutia hekima; Bali mwana aliyeachiliwa humwaibisha mamaye.
Matendo 3 : 19 โ 23
19 Tubuni basi, mrejee, ili dhambi zenu zifutwe, zipate kuja nyakati za kuburudishwa kwa kuwako kwake Bwana;
20 apate kumtuma Kristo Yesu mliyewekewa tangu zamani;
21 ambaye ilimpasa kupokewa mbinguni hata zije zamani za kufanywa upya vitu vyote, zilizonenwa na Mungu kwa kinywa cha manabii wake watakatifu tokea mwanzo wa ulimwengu.
22 Kwa maana Musa kweli alisema ya kwamba, Bwana Mungu wenu atawainulieni nabii, katika ndugu zenu, kama mimi; msikieni yeye katika mambo yote atakayonena nanyi.
23 Na itakuwa ya kwamba kila mtu asiyemsikiliza nabii huyo ataangamizwa na kutengwa na watu wake.
Waefeso 6 : 4
4 โก Nanyi, akina baba, msiwachokoze watoto wenu; bali waleeni katika adabu na maagizo ya Bwana.
Matendo 3 : 19 โ 21

Leave a Reply