Biblia inasema nini kuhusu kuhesabu baraka zako – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuhesabu baraka zako

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuhesabu baraka zako

2 Petro 3 : 9
9 ⑯ Bwana hakawii kuitimiza ahadi yake, kama wengine wanavyodhani anakawia, bali huwavumilia, maana hapendi mtu yeyote apotee, bali wote wafikie toba.

Zaburi 118 : 1 – 18
1 ③ Haleluya. Mshukuruni BWANA kwa kuwa ni mwema, Kwa maana fadhili zake ni za milele.
2 ④ Israeli na aseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
3 Mlango wa Haruni na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
4 Wamchao BWANA na waseme sasa, Ya kwamba fadhili zake ni za milele.
5 ⑤ Katika shida yangu nilimwita BWANA; BWANA akanijibu akaniweka panapo nafasi.
6 ⑥ BWANA yuko upande wangu, sitaogopa; Mwanadamu atanitenda nini?
7 ⑦ BWANA yuko upande wangu, msaidizi wangu, Kwa hiyo nitawaona wanaonichukia wakiwa wameshindwa.
8 ⑧ Ni heri kumkimbilia BWANA Kuliko kuwatumainia wanadamu.
9 ⑩ Ni heri kumkimbilia BWANA. Kuliko kuwatumainia wakuu.
10 Mataifa yote walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
11 ⑪ Walinizunguka, naam, walinizunguka; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
12 ⑫ Walinizunguka kama nyuki, Walizimika kama moto wa miibani; Kwa jina la BWANA niliwakatilia mbali.
13 Ulinisukuma sana ili nianguke; Lakini BWANA akanisaidia.
14 ⑬ BWANA ni nguvu zangu na wimbo wangu, Naye amekuwa wokovu wangu.
15 Sauti ya furaha na wokovu Imo hemani mwao wenye haki; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
16 ⑭ Mkono wa kulia wa BWANA umetukuzwa; Mkono wa kulia wa BWANA hutenda makuu.
17 ⑮ Sitakufa bali nitaishi, Nami nitayasimulia matendo ya BWANA.
18 ⑯ BWANA ameniadhibu sana, Lakini hakuniacha nife.

Zaburi 103 : 2
2 Ee nafsi yangu, umhimidi BWANA, Wala usizisahau fadhili zake zote.

Mwanzo 12 : 1
1 BWANA akamwambia Abramu, Toka wewe katika nchi yako, na jamaa zako, na nyumba ya baba yako, uende mpaka nchi nitakayokuonesha;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *