Biblia inasema nini kuhusu Kuhani – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kuhani

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuhani

Mwanzo 14 : 18
18 Na Melkizedeki mfalme wa Salemu akaleta mkate na divai, naye alikuwa kuhani wa Mungu Aliye Juu Sana.

Waraka kwa Waebrania 5 : 6
6 Kama asemavyo mahali pengine, Ndiwe kuhani milele Kwa mfano wa Melkizedeki.

Waraka kwa Waebrania 5 : 11
11 Yeye ambaye tuna maneno mengi ya kunena kuhusu habari zake; na ni shida kuyaeleza kwa kuwa mmekuwa wavivu wa kusikia.

Waraka kwa Waebrania 6 : 20
20 ① alimoingia Yesu kwa ajili yetu, mtangulizi wetu, amekuwa kuhani mkuu hata milele kwa mfano wa Melkizedeki.

Waraka kwa Waebrania 7 : 21
21 ⑧ (maana wale walifanywa makuhani pasipo kiapo; bali yeye, pamoja na kiapo, kwa yeye aliyemwambia, Bwana ameapa wala hataghairi, Wewe u kuhani milele;)

Kutoka 2 : 16
16 Basi kuhani wa Midiani alikuwa na binti saba, nao wakaja wakateka maji, wakazijaza birika maji, wapate kunywesha kundi la baba yao.

Kutoka 19 : 22
22 ⑫ Makuhani nao, wamkaribiao BWANA, na wajitakase, BWANA asije akawakasirikia.

Kutoka 19 : 24
24 BWANA akamwambia, Nenda, ushuke wewe; nawe utakwea, wewe, na Haruni pamoja nawe; lakini wale makuhani na watu wasipenye kumkaribia BWANA, asije yeye akawafurikia juu yao.

Mhubiri 5 : 6
6 Usikiache kinywa chako kuukosesha mwili wako; wala usiseme mbele ya huyo malaika ya kwamba hukukusudia; kwa nini Mungu akasirishwe na maneno yako, na kuiharibu kazi ya mikono yako?

Kutoka 28 : 4
4 Na mavazi watakayoyafanya ni haya; kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo; na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Haruni nduguyo, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.

Kutoka 29 : 9
9 Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.

Kutoka 29 : 44
44 Nami nitaitakasa hiyo hema ya kukutania, na hiyo madhabahu; pia Haruni na wanawe nitawatakasa, ili wanitumikie katika kazi ya ukuhani.

Hesabu 3 : 10
10 Nawe utawaweka Haruni na wanawe, nao wataushika ukuhani wao, na mgeni atakayekaribia atauawa.

Hesabu 18 : 7
7 Nawe na wanao pamoja nawe mtautunza ukuhani wenu, kwa ajili ya kila kitu cha madhabahu, na kwa ajili ya vile vilivyomo ndani ya pazia, nanyi mtatumika. Nawapeni ukuhani kuwa utumishi wa kipawa; na mgeni akaribiaye atauawa.

1 Mambo ya Nyakati 23 : 13
13 Wana wa Amramu; Haruni na Musa; naye Haruni akatengwa, ili ayatakase yaliyo matakatifu sana, yeye na wanawe milele, ili kufukiza uvumba mbele za BWANA, kumtumikia, na kubariki kwa jina lake, milele.

Kutoka 27 : 21
21 ⑳ Ndani ya ile hema ya kukutania, nje ya hilo pazia, lililo mbele ya huo ushuhuda, Haruni na wanawe wataitengeza tangu jioni hadi asubuhi mbele ya BWANA; itakuwa ni amri ya milele katika vizazi vyao vyote kwa ajili ya wana wa Israeli.

Kutoka 28 : 43
43 na Haruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.

Kutoka 29 : 9
9 Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.

Kutoka 29 : 9
9 Nawe uwakaze mishipi, Haruni na wanawe, na kuwavika kofia; nao watakuwa na huo ukuhani kwa amri ya milele; nawe utawaweka Haruni na wanawe kwa kazi takatifu.

Kutoka 29 : 35
35 ⑱ Ni hivyo utakavyowatendea Haruni na wanawe, sawasawa na hayo yote niliyokuagiza; utawaweka kwa kazi takatifu siku saba.

Kutoka 40 : 16
16 Musa akafanya hayo yote; kama BWANA aliyoagiza ndivyo alivyofanya yote.

Mambo ya Walawi 6 : 23
23 Tena kila sadaka ya unga ya kuhani itateketezwa kabisa; isiliwe.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *