Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kufuma
Isaya 19 : 9
9 Tena wao wafanyao kazi ya kuchana kitani watafadhaika, na hao pia wafumao bafta.
Isaya 38 : 12
12 ⑱ Makao yangu yameondolewa kabisa, yamechukuliwa kama hema ya mchungaji; Nimekunja maisha yangu kama mfumaji; atanikatilia mbali na kitanda cha mfumi; Tangu mchana hata usiku wanimaliza.
Kutoka 35 : 35
35 ⑪ Amewajaza watu hao ujuzi, ili watumike katika kazi za kila aina, mawe, na kazi ya fundi mwenye kutia taraza, katika nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri, ya mwenye kufuma nguo; ya hao wafanyao kazi yoyote, na ya wenye kuvumbua kazi za werevu.
2 Wafalme 23 : 7
7 ⑫ Akaziangusha nyumba za mahanithi, waliokuwamo nyumbani mwa BWANA, wanawake walipofuma mapazia ya Ashera.
Kutoka 28 : 32
32 Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma,[32] ili lisipasuke.
Kutoka 39 : 22
22 ⑮ Naye akafanya hilo joho la naivera ya kazi ya kusuka, rangi ya samawati yote;
Kutoka 39 : 27
27 ⑰ Nao wakafanya hizo kanzu za nguo ya kitani nzuri ya kufumwa, kwa Haruni, na kwa wanawe
Ayubu 7 : 6
6 Siku zangu hupita upesi kuliko chombo cha kufumia, Nazo zapita pasipokuwa na matumaini.
Waamuzi 16 : 14
14 Basi akazifunga kwa msumari, akamwambia Samsoni, Wafilisti wanakujia. Naye akaamka usingizini, akaung’oa ule msumari, na ule mtande.
2 Samweli 21 : 19
19 Kulikuwa na vita tena na Wafilisti huko Gobu; na Elhanani, mwana wa Yairi, Mbethlehemi, alimwua Goliathi, Mgiti, ambaye mpini wa mkuki wake ulikuwa kama mpini wa mfuma nguo
1 Mambo ya Nyakati 11 : 23
23 Huyo akamwua Mmisri, mtu mrefu sana, aliyekuwa wa dhiraa tano urefu wake; na yule Mmisri alikuwa na mkuki kama mti wa mfumaji mkononi; lakini yeye akamshukia na gongo, akamnyakulia Mmisri mkuki mkononi, akamwua kwa mkuki wake mwenyewe.
Leave a Reply