Biblia inasema nini kuhusu kufichua siri – Mistari yote ya Biblia kuhusu kufichua siri

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kufichua siri

1 Wakorintho 2 : 10
10 ⑤ Lakini Mungu ametufunulia sisi kwa Roho. Maana Roho huchunguza yote, hata mafumbo ya Mungu.

Mithali 11 : 13
13 Mwenye udaku hupitapita akifunua siri; Bali mwenye roho ya uaminifu husitiri mambo.

1 Petro 2 : 1 – 25
1 Basi, wekeni mbali uovu wote na hila yote, na unafiki na husuda na masingizio yote.
2 Kama watoto wachanga waliozaliwa sasa yatamanini maziwa ya akili yasiyoghoshiwa, ili kwa hayo mpate kuukulia wokovu;
3 ① ikiwa mmeonja ya kwamba Bwana ni mwenye fadhili.
4 ② Mmwendee yeye, jiwe lililo hai, lililokataliwa na wanadamu, bali kwa Mungu ni teule, lenye heshima.
5 ③ Ninyi nanyi, kama mawe yaliyo hai, mmejengwa muwe nyumba ya Roho, ukuhani mtakatifu, mtoe dhabihu za roho, zinazokubaliwa na Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo.
6 ④ Kwa kuwa imeandikwa katika Maandiko: Tazama, naweka katika Sayuni jiwe kuu la pembeni, teule, lenye heshima, Na kila amwaminiye hatatahayarika.
7 ⑤ Basi, heshima hii ni kwenu ninyi mnaoamini. Bali kwao wasioamini, Jiwe walilolikataa waashi, Limekuwa jiwe kuu la pembeni.
8 ⑥ Tena, Jiwe la kujikwaza mguu, na mwamba wa kuangusha. Kwa maana hujikwaza kwa neno lile, wasiliamini, nao waliwekwa kusudi wapate hayo.
9 ⑦ Bali ninyi ni uzao mteule, ukuhani wa kifalme, taifa takatifu, watu wa milki ya Mungu, mpate kuzitangaza fadhili zake yeye aliyewaita mtoke gizani mkaingie katika nuru yake ya ajabu;
10 ⑧ ninyi mliokuwa kwanza si taifa, bali sasa ni taifa la Mungu; mliokuwa hamkupata rehema, bali sasa mmepata rehema.
11 ⑩ Wapenzi, nawasihi kama wapitaji na wasafiri, ziepukeni tamaa za mwili zipiganazo na roho.
12 ⑪ Muwe na mwenendo mzuri kati ya Mataifa, ili, iwapo huwasingizia kuwa watenda mabaya, wayatazamapo matendo yenu mazuri, wamtukuze Mungu siku ya kujiliwa.
13 ⑫ Tiini kila kiamriwacho na watu, kwa ajili ya Bwana; iwe ni mfalme kama mwenye cheo kikubwa;
14 au iwe ni watawala, kama wanaotumwa naye ili kuwalipiza kisasi watenda mabaya na kuwasifu watenda mema.
15 ⑬ Kwa sababu ndiyo mapenzi ya Mungu, kwamba kwa kutenda mema mzibe vinywa vya ujinga vya watu wapumbavu;
16 ⑭ kama walio huru, ila wasioutumia uhuru huo kwa kusitiri ubaya, bali kama watumwa wa Mungu.
17 ⑮ Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.
18 ⑯ Enyi watumishi, watiini bwana zenu kwa hofu nyingi, sio wale walio wema na wenye upole tu, bali pia wale walio wakali.
19 Maana huu ndio wema hasa, mtu akivumilia huzuni kwa kumkumbuka Mungu, pale ateswapo pasipo haki.
20 ⑰ Kwa maana ni sifa gani kustahimili, mtendapo dhambi na kupigwa makofi? Lakini kustahimili, mtendapo mema na kupata mateso, huu ndio wema hasa mbele za Mungu.
21 ⑱ Kwa sababu ndio mlioitiwa; maana Kristo naye aliteswa kwa ajili yenu, akawaachia kielelezo, mfuate nyayo zake.
22 ⑲ Yeye hakutenda dhambi, wala udanganyifu haukuwapo kinywani mwake.
23 ⑳ Yeye alipotukanwa, hakurudisha matukano; alipoteswa, hakutisha; bali alijikabidhi kwake yeye ahukumuye kwa haki.
24 Yeye mwenyewe alizichukua dhambi zetu katika mwili wake juu ya mti, tukiwa wafu kwa mambo ya dhambi, tuwe hai kwa mambo ya haki; na kwa kupigwa kwake mliponywa.
25 Kwa maana mlikuwa mnapotea kama kondoo; lakini sasa mmemrudia Mchungaji na Mwangalizi wa roho zenu.

Amosi 3 : 7
7 Hakika Bwana MUNGU hatafanya neno lolote, bila kuwafunulia watumishi wake manabii siri yake.

Waraka kwa Waebrania 10 : 16 – 20
16 ③ Hili ni agano nitakaloagana nao baada ya siku zile, anena Bwana, Nitatia sheria zangu mioyoni mwao, Na katika fikira zao nitaziandika; ndipo anenapo,
17 ④ Dhambi zao na uasi wao sitaukumbuka tena kabisa.
18 Basi, ondoleo la hayo likiwapo, hapana toleo tena kwa ajili ya dhambi.
19 ⑤ Basi, ndugu, kwa kuwa tuna ujasiri wa kupaingia patakatifu kwa damu ya Yesu,
20 ⑥ njia ile aliyotuanzia iliyo mpya, iliyo hai, ipitayo katika pazia, yaani, mwili wake;

1 Mambo ya Nyakati 2 : 1 – 55
1 ② Hawa ndio wana wa Israeli; Reubeni, na Simeoni, na Lawi, na Yuda, na Isakari, na Zabuloni;
2 ③ na Dani, na Yusufu, na Benyamini, na Naftali, na Gadi, na Asheri.
3 Wana wa Yuda; Eri, na Onani, na Shela; ambao hao watatu alizaliwa na binti Shua, Mkanaani. Naye Eri, mzaliwa wa kwanza wa Yuda, alikuwa mbaya machoni pa BWANA; naye akamwua.
4 ④ Na Tamari, mkwewe, akamzalia Peresi, na Zera. Wana wote wa Yuda ni watano.
5 ⑤ Wana wa Peresi; Hesroni, na Hamuli.
6 ⑥ Na wana wa Zera; Zabdi, na Ethani, na Hemani, na Kalkoli, na Darda; hao wote ni watano.
7 ⑦ Na wana wa Karmi; Akani, yule aliyewataabisha Israeli, kwa kuchukua kilichowekwa wakfu.
8 Na wana wa Ethani; Azaria.
9 ⑧ Tena wana wa Hesroni aliozaliwa; Yerameeli, na Ramu, na Kalebu.
10 ⑩ Na Ramu akamzaa Aminadabu; na Aminadabu akamzaa Nashoni, mkuu wa wana wa Yuda;
11 ⑪ na Nashoni akamzaa Salmoni; na Salmoni akamzaa Boazi;
12 na Boazi akamzaa Obedi; na Obedi akamzaa Yese;
13 ⑫ na Yese akamzaa Eliabu, mzaliwa wake wa kwanza, na wa pili Abinadabu, na wa tatu Shama;
14 na wa nne Nethaneli, na wa tano Radai;
15 na wa sita Ozemu, na wa saba Daudi;
16 ⑬ na dada zao ni Seruya, na Abigaili. Na wana wa Seruya walikuwa, Abishai, na Yoabu, na Asaheli; hao watatu.
17 ⑭ Na Abigaili akamzaa Amasa; na babaye Amasa ni Yetheri, Mwishmaeli.
18 Basi Kalebu, mwana wa Hesroni, akazaliwa wana na mkewe Azuba, na Yeriothi, na hawa ndio wanawe wa kiume; Yesheri, na Shobabu, na Ardoni.
19 Akafa Azuba, naye Kalebu akamtwaa Efrata, aliyemzalia Huri.
20 ⑮ Naye Huri akamzaa Uri; na Uri akamzaa Besaleli.
21 ⑯ Na baadaye Hesroni akamwingilia binti wa Makiri, babaye Gileadi; ambaye alimtwaa alipokuwa na umri wa miaka sitini; naye akamzalia Segubu.
22 Na Segubu akamzaa Yairi, aliyekuwa mwenye miji ishirini na mitatu katika nchi ya Gileadi.
23 ⑰ Na Geshuri na Aramu wakawapokonya miji ya Yairi, pamoja na Kenathi na miji yake, jumla yote miji sitini. Hao wote ni wana wa Makiri, babaye Gileadi.
24 ⑱ Tena, baada ya kufa kwake Hesroni huko Kalebu-Efrata, ndipo Abia, mkewe Hesroni, alipomzalia Ashuri, babaye Teboa.
25 Na wana wa Yerameeli, mzaliwa wa kwanza wa Hesroni, walikuwa Ramu, mzaliwa wa kwanza, na Buna, na Oreni, na Ozemu; kwa Ahiya.
26 Naye Yerameeli alikuwa na mke mwingine, jina lake Atara; yeye alikuwa mamaye Onamu.
27 Na wana wa Ramu, mzaliwa wa kwanza wa Yerameeli, walikuwa Maasi, na Yamini, na Ekeri.
28 Na wana wa Onamu walikuwa Shamai, na Yada; na wana wa Shamai; Nadabu, na Abishuri.
29 Na mkewe Abishuri aliitwa jina lake Abihaili; naye akamzalia Abani, na Molidi.
30 Na wana wa Nadabu; Seledi, na Apaimu; lakini Seledi alipokufa hakuwa na watoto.
31 Na wana wa Apaimu; Ishi. Na wana wa Ishi; Sheshani. Na wana wa Sheshani; Alai.
32 Na wana wa Yada, nduguye Shamai; Yetheri, na Yonathani; naye Yetheri alipokufa hakuwa na watoto.
33 Na wana wa Yonathani; Pelethi, na Zaza. Hao ndio wana wa Yerameeli.
34 Basi huyo Sheshani alikuwa hana wana wa kiume, ila binti. Naye Sheshani alikuwa na mtumwa, Mmisri, jina lake akiitwa Yarha.
35 Basi akamwoza binti yake aolewe na Yarha, mtumwa wake; naye akamzalia Atai.
36 ⑲ Na Atai akamzaa Nathani; na Nathani akamzaa Zabadi;
37 na Zabadi akamzaa Eflali; na Eflali akamzaa Obedi;
38 na Obedi akamzaa Yehu; na Yehu akamzaa Azaria;
39 na Azaria akamzaa Helesi; na Helesi akamzaa Eleasa
40 na Eleasa akamzaa Sismai; na Sismai akamzaa Shalumu;
41 na Shalumu akamzaa Yekamia; na Yekamia akamzaa Elishama.
42 Na wana wa Kalebu, nduguye Yerameeli, walikuwa Mesha, mzaliwa wake wa kwanza, aliyekuwa babaye Zifu; na wana wa Maresha, babaye Hebroni.
43 Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.
44 Naye Shema akamzaa Rahamu, babaye Yorkeamu; na Rekemu akamzaa Shamai.
45 Na mwana wake Shamai alikuwa Maoni; na Maoni alikuwa babaye Beth-suri.
46 Naye Efa, suria yake Kalebu, alimzaa Harani, na Mosa, na Gazezi; naye Harani akamzaa Gazezi.
47 Na wana wa Yadai; Regemu, na Yothamu, na Geshani, na Peleti, na Efa, na Shaafu.
48 Naye Maaka, suria yake Kalebu, akamzalia Sheberi, na Tirhana.
49 ⑳ Tena akamzaa Shaafu, babaye Madmana; na Sheva babaye Makbena; na babaye Gibea; naye binti Kalebu alikuwa Aksa.
50 Hao walikuwa wana wa Kalebu. Wana wa Huri, mzaliwa wa kwanza wa Efrata; Shobali, babaye Kiriath-Yearimu;
51 Salma, babaye Bethlehemu; na Harefu, babaye Beth-gaderi.
52 Naye Shobali, babaye Kiriath-Yearimu, alikuwa na wana; Haroe, na nusu ya Wamenuhothi.
53 Na jamaa za Kiriath-Yearimu; Waithri, na Waputhi, na Washumathi, na Wamishrai; katika hao walitoka Wasorathi, na Waeshtaoli.
54 Na wana wa Salma; Bethlehemu, na Wanetofathi, Atroth-beth-Yoabu, na nusu ya Wamenuhothi, na Wazori.
55 Na jamaa za waandishi waliokaa Yabesi; Watirathi, na Washimeathi, na Wasukathi. Hao ndio Wakeni, waliotoka kwake Hamathi, babaye mbari ya Rekabu.

Sefania 1 : 18
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya BWANA; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, mwisho wa kutisha.

1 Timotheo 2 : 1 – 15
1 Basi, kabla ya mambo yote, nataka dua, na sala, na maombezi, na shukrani, zifanyike kwa ajili ya watu wote;
2 kwa ajili ya wafalme na wote wenye mamlaka, tuishi maisha ya utulivu na amani, katika utauwa wote na ustahivu.
3 Hili ni zuri, nalo lakubalika mbele za Mungu Mwokozi wetu;
4 ambaye hutaka watu wote waokolewe, na kupata kujua yaliyo kweli.
5 Kwa sababu Mungu ni mmoja, na mpatanishi kati ya Mungu na wanadamu ni mmoja, Mwanadamu Kristo Yesu;
6 ambaye alijitoa mwenyewe kuwa ukombozi kwa ajili ya wote, utakaoshuhudiwa kwa majira yake.
7 Nami kwa ajili ya huo niliwekwa niwe mhubiri na mtume, (nasema kweli, sisemi uongo), mwalimu wa Mataifa katika imani na kweli.
8 Basi, nataka wanaume waombe kila mahali, huku wakiinua mikono iliyotakata pasipo hasira wala majadiliano.
9 Vivyo hivyo wanawake na wajipambe kwa mavazi ya kujisitiri, pamoja na adabu nzuri, na moyo wa kiasi; si kwa kusuka nywele, wala kwa dhahabu na lulu, wala kwa nguo za thamani;
10 bali kwa matendo mema, kama iwapasavyo wanawake wanaoukiri uchaji wa Mungu.
11 Mwanamke na ajifunze katika utulivu, akitii kwa kila namna.
12 Simpi mwanamke ruhusa ya kufundisha, wala kumtawala mwanamume, bali awe msikivu.
13 ① Kwa maana Adamu ndiye aliyeumbwa kwanza, na Hawa baadaye.
14 ② Wala Adamu hakudanganywa, ila mwanamke alidanganywa kabisa akaingia katika hali ya kukosa.
15 Lakini ataokolewa kwa kuzaa kwake, kama wakidumu katika imani na upendo na utakaso, pamoja na moyo wa kiasi.

Wakolosai 1 : 26
26 siri ile iliyofichwa tangu zamani zote na tangu vizazi vyote, bali sasa imefunuliwa kwa watakatifu wake;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *