Biblia inasema nini kuhusu kuchukua hatua – Mistari yote ya Biblia kuhusu kuchukua hatua

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kuchukua hatua

Yakobo 2 : 14 – 17
14 ① Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,
16 ② na mmoja wenu akawaambia, Nendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya kimwili, yafaa nini?
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.

Yakobo 1 : 23 – 25
23 Kwa sababu mtu akiwa ni msikiaji wa neno tu, wala si mtendaji, mtu huyo ni kama mtu anayejiangalia uso wake katika kioo.
24 Maana hujiangalia, kisha huenda zake, mara akasahau jinsi alivyo.
25 Lakini aliyeitazama sheria kamilifu iliyo ya uhuru, na kukaa humo, asiwe msikiaji msahaulifu, bali mtendaji wa kazi, huyo atakuwa heri katika kutenda kwake.

Yakobo 2 : 18
18 ③ Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.

2 Petro 1 : 5 – 8
5 Naam, na kwa sababu iyo hiyo jitahidini sana ili katika imani yenu mtie na wema, na katika wema wenu maarifa,
6 na katika maarifa yenu kiasi, na katika kiasi chenu subira, na katika subira yenu utauwa,
7 na katika utauwa wenu upendano wa ndugu, na katika upendano wa ndugu, upendo.
8 Maana mambo hayo yakiwa kwenu na kujaa tele, yawafanya ninyi kuwa si wavivu wala si watu wasio na matunda, kwa kumjua Bwana wetu Yesu Kristo.

Wakolosai 3 : 23 – 24
23 Lolote mfanyalo, lifanyeni kwa moyo, kama kwa Bwana, wala si kwa wanadamu,
24 mkijua ya kuwa mtapokea kwa Bwana ujira wa urithi. Mnamtumikia Bwana Kristo.

1 Yohana 3 : 18
18 Watoto wadogo, tusipende kwa neno, wala kwa ulimi, bali kwa tendo na kweli.

Luka 11 : 9
9 ⑪ Nami nawaambia, Ombeni, nanyi mtapewa; tafuteni, nanyi mtaona; bisheni, nanyi mtafunguliwa.

1 Petro 1 : 13
13 Kwa hiyo iweni tayari, na makini;[1] mkiitumainia kwa utimilifu ile neema mtakayoletewa katika ufunuo wake Yesu Kristo.

2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Waefeso 6 : 10 – 18
10 ⑥ Hatimaye, mzidi kuwa hodari katika Bwana na katika uweza wa nguvu zake.
11 ⑦ Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za Shetani.
12 ⑧ Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho.
13 ⑩ Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu, na mkiisha kuyatimiza yote, kusimama.
14 ⑪ Basi simameni, mkiwa mmejifunga kweli viunoni, na kuvaa dirii ya haki kifuani,
15 ⑫ na kama viatu vilivyofungiwa miguuni mwenu muwe tayari kutangaza Injili ya amani;
16 ⑬ zaidi ya yote mkiitwaa ngao ya imani, ambayo kwa hiyo mtaweza kuizima mishale yote yenye moto ya yule mwovu.
17 ⑭ Tena ipokeeni chapeo ya wokovu, na upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu;
18 ⑮ kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote;

1 Timotheo 6 : 18 – 19
18 Waamuru watende mema, wawe matajiri katika kutenda mema, wawe wakarimu na wawe tayari kushiriki na wengine;
19 ② huku wakijiwekea akiba iwe msingi mzuri kwa wakati ujao, ili wapate uzima ulio kweli kweli.

Waraka kwa Waebrania 6 : 11 – 12
11 Nasi twataka sana kila mmoja wenu aidhihirishe bidii ile ile, kwa utimilifu wa matumaini hata mwisho;
12 ili msiwe wavivu, bali mkawe kama hao wazirithio ahadi kwa imani na uvumilivu.

Luka 10 : 33 – 37
33 ③ Lakini, Msamaria mmoja katika kusafiri kwake alifika hapo alipokuwa; na alipomwona alimhurumia,
34 akakaribia, akamfunga majeraha yake, akayatia mafuta na divai; akampandisha juu ya mnyama wake, akampeleka mpaka nyumba ya wageni, akamtunza.
35 Hata siku ya pili akatoa dinari mbili, akampa mwenye nyumba ya wageni, akisema, Mtunze huyu, na chochote utakachogharimiwa zaidi, mimi nitakaporudi nitakulipa.
36 Waonaje wewe, katika hao watatu, ni yupi aliyekuwa jirani yake yule aliyeangukia kati ya wanyang’anyi?
37 Akasema, Ni huyo aliyemwonea huruma. Yesu akamwambia, Nenda zako, nawe ukafanye vivyo hivyo.

Mithali 27 : 23
23 Fanya bidii kuijua hali ya makundi yako; Na kuwaangalia sana ng’ombe wako.

Yakobo 1 : 5
5 Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

2 Wafalme 7 : 3 – 8
3 Basi walikuwapo watu wanne wenye ukoma, penye lango la mji; wakasemezana, Mbona tunakaa hapa hata tufe?
4 Tukisema, Tutaingia mjini, mjini mna njaa, nasi tutakufa humo; nasi tukikaa hapa, tutakufa vile vile. Haya! Twende tukaliendee jeshi la Washami; wakituhifadhi hai tutaishi; wakituua, tutakufa tu.
5 Basi wakaondoka kabla ya mapambazuko, ili waende mpaka kituo cha Washami; na walipofika mwanzo wa kambi ya Washami, kumbe! Hapakuwa na mtu.
6 Kwa maana Bwana alikuwa amewasikizisha Washami kishindo cha miendo ya magari, na kishindo cha farasi, kama kishindo cha jeshi kubwa; wakaambiana, Tazama, mfalme wa Israeli amewaajiri wafalme wa Wahiti, na wafalme wa Wamisri, waje wapigane nasi.
7 Kwa hiyo wakaondoka, wakakimbia kungali giza bado, wakaziacha hema zao, na farasi wao, na punda zao, na kambi yao vile vile kama ilivyokuwa, wakakimbia wapate kujiponya nafsi zao.
8 Basi wale wenye ukoma walipofika mwisho wa kituo, waliingia katika hema moja, wakala, na kunywa, wakachukua fedha, na dhahabu, na mavazi, wakaenda wakavificha; wakarudi, wakaingia katika hema ya pili, vile vile wakachukua vitu, wakaenda, wakavificha.

Wakolosai 3 : 2
2 Yafikirini yaliyo juu, siyo yaliyo katika nchi.

Danieli 11 : 32
32 Na wao wafanyao maovu juu ya hilo agano atawapotosha kwa maneno ya kujipendekeza; lakini watu wamjuao Mungu wao watakuwa hodari, na kutenda mambo makuu.

Zaburi 119 : 60
60 Nilifanya haraka wala sikukawia, Kuyatii maagizo yako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *