Biblia inasema nini kuhusu Kuasili – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kuasili

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kuasili

Mwanzo 15 : 3
3 Abramu akasema, Tazama, hukunipa uzao, na mtumwa aliyezaliwa nyumbani mwangu ndiye mrithi wangu.

Mwanzo 48 : 5
5 ⑳ Basi sasa wanao wawili uliozaliwa katika nchi ya Misri kabla sijaja kwako Misri ni watoto wangu, yaani, Efraimu na Manase watakuwa wangu, kama Reubeni na Simeoni.

Mwanzo 48 : 14
14 Israeli akanyosha mkono wake wa kulia akauweka juu ya kichwa cha Efraimu, aliyekuwa mdogo, na mkono wake wa kushoto akauweka juu ya kichwa cha Manase, huku akijua atiavyo mikono; maana Manase ndiye aliyezaliwa kwanza.

Mwanzo 48 : 16
16 naye Malaika aliyeniokoa na maovu yote, na awabariki vijana hawa; jina langu na litajwe juu yao, na jina la baba zangu, Abrahamu na Isaka; na wawe wingi wa watu kati ya nchi.

Mwanzo 48 : 22
22 Nami nimekupa wewe sehemu moja zaidi kuliko ndugu zako, niliyoitwaa katika mikono ya Waamori, kwa upanga wangu na upinde wangu.

Kutoka 2 : 10
10 Mtoto akakua, naye akamleta kwa binti Farao, akawa mwanawe. Akamwita jina lake Musa.[1]

Matendo 7 : 21
21 ⑲ Wakati alipotupwa, binti Farao akamtwaa, akamlea awe kama mwanawe.

Waraka kwa Waebrania 11 : 24
24 Kwa imani Musa alipokuwa mtu mzima, akakataa kuitwa mwana wa binti Farao;

Esta 2 : 7
7 Naye alikuwa amemlea Hadasa, yaani, Esta, binti wa mjomba wake, kwa kuwa hana baba wala mama. Naye msichana huyu alikuwa wa umbo nzuri na uso mwema; nao walipokufa baba yake na mama yake, yule Mordekai alimtwaa kuwa binti yake.

Kutoka 4 : 23
23 nami nimekuambia, Mpe mwanangu ruhusa aende, ili apate kunitumikia, nawe umekataa kumpa ruhusa aende; angalia basi, mimi nitamwua mwanao, mzaliwa wa kwanza wako.

Hesabu 6 : 27
27 ⑭ Ndivyo watakavyoweka jina langu juu ya wana wa Israeli; nami nitawabariki.

Kumbukumbu la Torati 28 : 10
10 Na mataifa yote ya duniani watakuona umeitwa kwa jina la BWANA, nao watakuwa na hofu kwako.

2 Mambo ya Nyakati 7 : 14
14 ikiwa watu wangu, walioitwa kwa jina langu, watajinyenyekeza, na kuomba, na kunitafuta uso, na kuziacha njia zao mbaya; basi, nitasikia toka mbinguni, na kuwasamehe dhambi yao, na kuiponya nchi yao.

Isaya 43 : 7
7 Kila mmoja aliyeitwa kwa jina langu, niliyemwumba kwa ajili ya utukufu wangu; mimi nimemwumba, naam, mimi nimemfanya.

Kumbukumbu la Torati 14 : 1
1 Ninyi mmekuwa wana wa BWANA, Mungu wenu; msijitoje miili yenu, wala msifanye upaa katikati ya macho yenu kwa ajili ya aliyekufa.

Kumbukumbu la Torati 26 : 18
18 naye BWANA amekuungama hivi leo kuwa taifa iliyotengwa iwe yake yeye, kama alivyokuahidi, na kuwa yakupasa kushika maagizo yake yote;

Kumbukumbu la Torati 27 : 9
9 Musa na makuhani Walawi wakawaambia Israeli wote wakasema, Nyamaza, usikize, Ee Israeli; leo umekuwa watu wa BWANA, Mungu wako.

Kumbukumbu la Torati 32 : 6
6 Je! Mnamlipa BWANA hivi, Enyi watu wapumbavu na ujinga? Je! Yeye siye baba yako aliyekununua? Amekufanya, na kukuweka imara.

2 Samweli 7 : 14
14 Mimi nitakuwa baba yake, naye atakuwa mwanangu; akitenda maovu nitamwadhibu kwa fimbo ya binadamu na kwa mapigo ya wanadamu;

1 Mambo ya Nyakati 22 : 10
10 ⑭ huyo ndiye atakayejenga nyumba kwa ajili ya jina langu; naye atakuwa mwanangu, nami nitakuwa babaye; nami nitakiimarisha milele kiti cha ufalme wake juu ya Israeli.

1 Mambo ya Nyakati 28 : 6
6 ④ Akaniambia, Sulemani, mwanao, ndiye atakayeijenga nyumba yangu na nyua zangu; kwa kuwa nimemchagua awe mwanangu, nami nitakuwa babaye.

Mithali 14 : 26
26 Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.

Isaya 8 : 18
18 ② Angalieni, mimi na watoto hawa niliopewa na BWANA tu ishara na ajabu katika Israeli, zitokazo kwa BWANA wa majeshi, yeye akaaye katika mlima Sayuni.

Isaya 43 : 6
6 nitaiambia kaskazi, Toa; nayo kusi, Usizuie; waleteni wana wangu kutoka mbali, na binti zangu kutoka miisho ya dunia.

Isaya 63 : 1 – 232

1 ④ Ni nani huyu atokaye Edomu, Atokaye Bosra akiwa na mavazi yenye madoa mekundu? Huyu aliye na nguo za fahari, Anayekwenda katika ukuu wa uweza wake? Ndimi nisemaye kwa haki, Niliye hodari wa kuokoa.
2 ⑤ Kwa nini mavazi yako ni mekundu, Na nguo zako kama za mtu akanyagaye zabibu?
3 ⑥ Nilikanyaga shinikizoni peke yangu; Wala katika watu hakuwapo mtu pamoja nami; Naam, niliwakanyaga kwa hasira yangu, Niliwaponda kwa ghadhabu yangu; Na mavazi yangu yametiwa madoa kwa damu yao, Nami nimezichafua nguo zangu zote.
4 Maana siku ya kisasi ilikuwamo moyoni mwangu, Na mwaka wao niliowakomboa umewadia.
5 ⑦ Nikatazama, wala hapakuwa na wa kunisaidia; Nikashangaa kwa kuwa hakuna mwenye kutegemeza; Basi, mkono wangu mwenyewe uliniletea wokovu, Ghadhabu yangu ndiyo iliyonitegemeza.
6 ⑧ Nikayakanyaga makabila ya watu kwa hasira yangu, Nikawalevya kwa ghadhabu yangu, Nami nikaimwaga damu yao chini.
7 Nitautaja wema wa BWANA, sifa za BWANA kwa yote aliyotukirimia BWANA; na wingi wa wema wake kwa nyumba ya Israeli, aliowakirimia kwa rehema zake, na kwa wingi wa wema wake.
8 Maana alisema, Hakika ndio watu wangu hawa, wana wasio na hila; akawa Mwokozi wao.
9 ⑩ Katika mateso yao yote yeye aliteswa, na malaika wa uso wake akawaokoa; kwa mapenzi yake, na huruma zake, aliwakomboa mwenyewe; akawainua, akawachukua siku zote za kale.
10 ⑪ Lakini wakaasi, wakamhuzunisha Roho yake Mtakatifu; kwa hiyo akawageukia, akawa adui, akapigana nao.
11 Ndipo alipozikumbuka siku za kale, za Musa, na watu wake, akisema, Yuko wapi yeye aliyewapandisha toka baharini pamoja na wachungaji wa kundi lake? Yuko wapi yeye aliyetia kati yao Roho yake Mtakatifu?
12 ⑫ Aliyewaongoza kwa mkono wake mtukufu, kwa mkono wa kulia wa Musa? Aliyeyatenga maji mbele yao, ili ajifanyie jina la milele?
13 Aliyewaongoza vilindini, kama farasi jangwani, wasijikwae?
14 Kama ng’ombe washukao bondeni, Roho ya BWANA ikawastarehesha; ndivyo ulivyowaongoza watu wako, ili ujifanyie jina lenye utukufu.
15 Tazama toka mbinguni, ukaone toka makao ya utukufu wako na fahari yako; uko wapi wivu wako, na uweza wako? Shauku ya moyo wako, na huruma zako zimezuiliwa kwangu.
16 ⑬ Maana wewe ndiwe Baba yetu, ijapokuwa Abrahamu hatujui, wala Israeli hatukiri; wewe, BWANA, ndiwe Baba yetu, mkombozi wetu tangu milele ndilo jina lako.
17 ⑭ Ee BWANA, mbona umetukosesha njia zako, ukatufanya kuwa na mioyo migumu hata tusikuogope? Urudi kwa ajili ya watumishi wako, makabila ya urithi wako.
18 ⑮ Watu wako watakatifu waliumiliki kwa kitambo tu; adui zetu wamepakanyaga patakatifu pako.
19 Tumekuwa kama watu usiowamiliki kamwe; kama watu wasioitwa kwa Jina lako.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *