Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kora
Mwanzo 36 : 5
5 Oholibama alizaa Yeushi, na Yalamu, na Kora. Hao ndio wana wa Esau aliozaliwa katika nchi ya Kanaani.
Mwanzo 36 : 14
14 Na hawa ni wana wa Oholibama, binti Ana, binti Sibeoni, mkewe Esau; akamzalia Esau, Yeushi, na Yalamu, na Kora.
Mwanzo 36 : 18
18 Na hawa ni wana wa Oholibama, mkewe Esau; jumbe Yeushi, jumbe Yalamu, jumbe Kora. Hao ndio majumbe waliotoka kwa Oholibama, binti Ana, mkewe Esau.
Kutoka 6 : 18
18 Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.
Kutoka 6 : 21
21 Na wana wa Ishari; ni Kora, na Nefegi, na Zikri.
Kutoka 6 : 24
24 Na wana wa Kora; ni Asiri, na Elkana, na Abiasafu; hizo ni jamaa za hao Wakora.
Hesabu 26 : 10
10 nchi ikafunua kinywa chake, na kuwameza pamoja na Kora, mkutano huo ulipokufa; wakati moto ulipowateketeza watu mia mbili na hamsini, nao wakawa ishara.
Kumbukumbu la Torati 11 : 6
6 ⑰ na alivyowafanya Dathani, na Abiramu, wana wa Eliabu mwana wa Reubeni; nchi ilivyofunua kinywa chake, ikawameza, na walio nyumbani mwao, na mahema yao, na kila kitu kilichokuwa hai kikiwafuata, katikati ya Israeli yote;
Zaburi 106 : 17
17 Nchi ikapasuka ikammeza Dathani, Ikaufunika mkutano wa Abiramu.
1 Mambo ya Nyakati 2 : 43
43 Na wana wa Hebroni; Kora, na Tapua, na Rekemu, na Shema.
1 Mambo ya Nyakati 6 : 22
22 Wana wa Kohathi; mwanawe huyo ni Ishari, na mwanawe huyo ni Kora, na mwanawe huyo ni Asiri;
Zaburi 42 : 11
11 Nafsi yangu, kwa nini kuinama, Na kufadhaika ndani yangu? Umtumaini Mungu; Kwa maana nitakuja kumsifu, Aliye afya ya uso wangu, Na Mungu wangu.
Leave a Reply