Biblia inasema nini kuhusu Kombe – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kombe

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kombe

Mwanzo 40 : 11
11 Na kikombe cha Farao kilikuwa mkononi mwangu, nikazitwaa zabibu, nikazikamua katika kikombe cha Farao, nikampa Farao kikombe mkononi mwake.

2 Samweli 12 : 3
3 bali yule maskini hakuwa na kitu, ila mwana-kondoo mmoja, mdogo, ambaye amemnunua na kumlea; naye akakua pamoja naye, na pamoja na wanawe; hula sehemu ya posho lake, na kukinywea kikombe chake, na kulala kifuani mwake, akawa kwake kama binti.

1 Wafalme 7 : 26
26 ⑬ Na unene wake ulikuwa nyanda nne; na ukingo wake ukafanywa kama ukingo wa kikombe, kama ua la yungi; huingia bathi[14] elfu mbili.

Mathayo 23 : 25
25 ⑰ Ole wenu Waandishi na Mafarisayo, wanafiki! Kwa kuwa mnasafisha nje ya kikombe na chano, na ndani yake vimejaa unyang’anyi na kutokuwa na kiasi.

Mwanzo 44 : 2
2 Na kikombe changu, kikombe kile cha fedha, ukitie kinywani mwa gunia la yule mdogo pamoja na fedha ya nafaka yake. Akafanya kama vile alivyomwambia Yusufu.

1 Mambo ya Nyakati 28 : 17
17 na nyuma, na mabakuli, na vikombe vya dhahabu safi; na kwa matasa ya dhahabu, kwa uzani kwa kila tasa; na kwa matasa ya fedha, kwa uzani kwa kila tasa;

Yeremia 52 : 19
19 Navyo vikombe, na vyombo vya kutolea majivu, na mabakuli, na masufuria, na vinara, na miiko, na vyetezo, vilivyokuwa vya dhahabu katika dhahabu, na vilivyokuwa vya fedha katika fedha, kamanda wa askari walinzi akavichukua.

Mathayo 26 : 27
27 Akakitwaa kikombe, akashukuru, akawapa, akisema, Kuyweni nyote katika hiki;

Marko 14 : 23
23 Akatwaa kikombe, akashukuru, akawapa; wakakinywea wote.

Luka 22 : 20
20 ⑬ Kikombe nacho vivyo hivyo baada ya kula; akisema, Kikombe hiki ni agano jipya katika damu yangu, inayomwagika kwa ajili yenu.]

1 Wakorintho 10 : 21
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

1 Wakorintho 10 : 21
21 Hamwezi kushirikiana katika meza ya Bwana na katika meza ya mashetani.

Zaburi 11 : 6
6 Awanyeshee wasio haki mitego, Moto na kiberiti na upepo wa joto Na viwe fungu la kikombe chao.

Zaburi 73 : 10
10 Kwa hiyo watu wake hugeuka huko, Na maji yaliyojaa humezwa nao.

Zaburi 75 : 8
8 ④ Maana mkononi mwa BWANA mna kikombe, Na mvinyo yake inatoka povu; Kumejaa machanganyiko; Naye huyamimina. Na sira zake wasio haki wa dunia Watazifyonza na kuzinywa.

Isaya 51 : 17
17 Amka, amka, simama, Ee Yerusalemu, Wewe uliyenywea mkononi mwa BWANA, Kikombe cha hasira yake; Ukalinywea na kumaliza bakuli la kulevyalevya Umelinywea na kulimaliza.

Isaya 51 : 22
22 BWANA, Bwana wako na Mungu wako, awateteaye watu wake, asema hivi, Tazama, nimeondoa mkononi mwako kikombe cha kulevyalevya, hilo bakuli la hasira yangu; hutalinywea tena;

Yeremia 25 : 28
28 Tena itakuwa, kama wakikataa kukipokea kikombe kile mkononi mwako, wanywe, ndipo utakapowaambia, BWANA wa majeshi asema hivi, Lazima mtakunywa.

Ezekieli 23 : 34
34 Naam, utakinywea hata hakitabaki kitu ndani yake, utavitafuna vigae vyake, utayararua maziwa yako; maana mimi, Bwana MUNGU, nimenena neno hili.

Mathayo 20 : 23
23 Akawaambia, Hakika mtakinywea kikombe changu; lakini kuketi mkono wangu wa kulia na mkono wangu wa kushoto, sina amri kuwapa, bali watapewa waliowekewa tayari na Baba yangu.

Mathayo 26 : 39
39 ⑯ Akaendelea mbele kidogo, akaanguka kifudifudi, akaomba, akisema, Baba yangu, ikiwezekana, kikombe hiki kiniondokee; lakini si kama nitakavyo mimi, bali kama utakavyo wewe.

Marko 14 : 36
36 ⑭ Akasema, Aba, Baba, yote yawezekana kwako; uniondolee kikombe hiki; lakini, si kama nitakavyo mimi, bali utakavyo wewe.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *