Biblia inasema nini kuhusu Kohathi – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kohathi

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kohathi

Mwanzo 46 : 11
11 Na wana wa Lawi; Gershoni, na Kohathi, na Merari.

Kutoka 6 : 16
16 Na haya ndiyo majina ya wana wa Lawi, kulingana na vizazi vyao; Gershoni,[9] na Kohathi, na Merari; na miaka ya maisha yake Lawi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na saba.

Hesabu 26 : 59
59 Na jina la mke wa Amramu aliitwa Yokebedi, binti wa Lawi, ambaye alizaliwa kwake Lawi huko Misri; na huyo Yokebedi akamzalia Amramu Haruni, na Musa, na Miriamu dada yao.

Kutoka 6 : 18
18 Na wana wa Kohathi; ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli; na miaka ya maisha ya huyo Kohathi ilikuwa ni miaka mia moja na thelathini na mitatu.

Hesabu 3 : 19
19 Na wana wa Kohathi kwa jamaa zao ni Amramu, na Ishari, na Hebroni, na Uzieli.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *