Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kivuli
Zaburi 57 : 1
1 Unirehemu, Ee Mungu, unirehemu mimi, Maana nafsi yangu imekukimbilia Wewe. Nitaukimbilia uvuli wa mbawa zako, Hadi misiba hii itakapopita.
Yakobo 1 : 17
17 Kila kutoa kuliko kwema, na kila kitolewacho kilicho kamili, hutoka juu, hushuka kwa Baba wa mianga; kwake hakuna kubadilika, wala kivuli cha kugeukageuka.
Wakolosai 2 : 16 – 17
16 ⑱ Basi, mtu asiwahukumu ninyi katika vyakula au vinywaji, au kwa sababu ya sikukuu au mwandamo wa mwezi, au sabato;
17 ⑲ mambo hayo ni kivuli cha mambo yajayo; bali mwili ni wa Kristo.
Leave a Reply