Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kitani
1 Wafalme 10 : 28
28 Nao farasi aliokuwa nao Sulemani wakaletwa toka Misri; wakapewa wafanya biashara wake mfalme kwa makundi, kila kundi na thamani yake.
Ezekieli 27 : 7
7 Tanga lako lilikuwa la kitani safi itokayo Misri, iliyotiwa taraza, ili iwe bendera kwako; na chandarua chako kilikuwa cha rangi ya samawati na urujuani toka visiwa vya Elisha.
Ezekieli 27 : 16
16 Shamu alikuwa mfanya biashara kwako, kwa sababu ya wingi wa kazi za mkono wako walifanya biashara kwa zumaridi, urujuani, kazi ya taraza, kitani safi, marijani na akiki, wapate vitu vyako vilivyouzwa.
Kutoka 26 : 1
1 Kisha fanya hiyo maskani iwe na mapazia kumi; ifanye ya nguo ya kitani nzuri ya kusokota, pamoja na nyuzi za rangi ya buluu, zambarau na nyekundu, pamoja na makerubi; kazi ya fundi stadi.
Kutoka 27 : 9
9 ⑱ Nawe fanya ua wa maskani; upande wa kusini wa kuelekea kusini kutakuwa na chandarua ya nguo ya kitani nzuri yenye kusokotwa, kwa huo ua, urefu wake upande mmoja utakuwa ni dhiraa mia moja;
Kutoka 28 : 8
8 Na mshipi stadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
Kutoka 28 : 15
15 Nawe utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera; ya nyuzi za dhahabu, za buluu, zambarau na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
Kutoka 28 : 42
42 Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hadi mapajani;
Mwanzo 41 : 42
42 Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Esta 8 : 15
15 ② Naye Mordekai akatoka usoni pa mfalme, amevaa mavazi ya kifalme, ya rangi ya samawati na nyeupe, mwenye taji kubwa la dhahabu, na joho la kitani safi na rangi ya zambarau. Mji wa Susa wakapaza sauti, wakashangilia.
Mwanzo 41 : 42
42 Farao akavua pete yake ya mhuri mkononi mwake, akaitia mkononi mwa Yusufu; akamvika mavazi ya kitani nzuri, na kumtia mkufu wa dhahabu shingoni mwake.
Ezekieli 9 : 2
2 Na tazama, watu sita wakaja, wakitokea kwa njia ya lango la juu, lielekealo upande wa kaskazini, kila mmoja akiwa na silaha yake ya kuua mkononi; na mtu mmoja kati yao akiwa amevaa bafta, naye ana kidau cha wino cha mwandishi kiunoni. Wakaingia, wakasimama karibu na madhabahu ya shaba.
Luka 16 : 19
19 Akasema, Palikuwa na mtu mmoja, tajiri, aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, na kula sikuzote kwa anasa.
Isaya 3 : 23
23 na vioo vidogo, na kitani nzuri, na vilemba, na utaji.
Ezekieli 16 : 13
13 Hivyo ulipambwa kwa dhahabu na fedha; na mavazi yako yalikuwa ya kitani safi, na hariri, na kazi ya taraza; ulikula unga mzuri, na asali, na mafuta; nawe ulikuwa mzuri mno, ukafanikiwa hata kufikia hali ya kifalme.
Mithali 7 : 16
16 Nimetandika kitanda changu, magodoro mazuri, Kwa matandiko ya Kimisri yenye mistari.
Mambo ya Walawi 19 : 19
19 Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja; wala usivae mwilini mwako nguo ya namna mbili zilizochanganywa pamoja.
Kumbukumbu la Torati 22 : 11
11 Usivae nguo iliyochanganyikana sufu na kitani pamoja.
Leave a Reply