Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kisiwa
Zaburi 97 : 1
1 BWANA ametamalaki, nchi na ishangilie, Visiwa vingi na vifurahi.
Isaya 11 : 11
11 Na itakuwa katika siku hiyo, Bwana atapeleka mkono wake mara ya pili, ili ajipatie watu wake watakaosalia, kutoka Ashuru, na kutoka Misri, na kutoka Pathrosi, na kutoka Kushi, na kutoka Elamu, na kutoka Shinari, na kutoka Hamathi, na kutoka visiwa vya bahari.
Isaya 41 : 1
1 Nyamazeni mbele zangu, enyi visiwa, na mataifa wajipatie nguvu mpya; na waje karibu wakanene; na tukaribiane pamoja kwa hukumu.
Isaya 41 : 5
5 Visiwa vimeona, vikaogopa; ncha za dunia zilitetemeka; walikaribia, walikuja.
Isaya 49 : 1
1 Nisikilizeni, enyi visiwa; tegeni masikio yenu, enyi makabila ya watu mlio mbali sana; BWANA ameniita tangu tumboni; toka tumbo la mama yangu amenitaja jina langu.
Sefania 2 : 11
11 BWANA atakuwa wa kutisha sana kwao; kwa maana atawaua kwa njaa miungu yote ya dunia; na watu watamsujudia yeye, kila mtu toka mahali pake; naam, nchi zote za mataifa.
Ufunuo 16 : 20
20 โญ Kila kisiwa kikakimbia, wala milima haikuonekana tena.
Leave a Reply