Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kishoni
Waamuzi 4 : 7
7 Nami nitakuvutia Sisera, kamanda wa jeshi la Yabini, hadi mto wa Kishoni, pamoja na magari yake, na wingi wa watu wake; nami nitamtia mkononi mwako.
Waamuzi 4 : 13
13 Sisera akayakusanya magari yake yote, naam, magari ya chuma mia tisa, na watu wote waliokuwa pamoja naye, toka Haroshethi wa Mataifa mpaka mto wa Kishoni.
Waamuzi 5 : 21
21 ⑯ Mto ule wa Kishoni uliwachukua, Ule mto wa zamani, mto wa Kishoni. Ee roho yangu, endelea mbele kwa nguvu.
Zaburi 83 : 9
9 ⑫ Uwatende kama ulivyowatenda Midiani, Sisera, Na Yabini, penye kijito cha Kishoni.
1 Wafalme 18 : 40
40 Eliya akawaambia, Wakamateni hao manabii wa Baali, asiokoke hata mmoja. Wakawakamata; na Eliya akawachukua mpaka kijito cha Kishoni, akawaua huko.
Leave a Reply