Biblia inasema nini kuhusu Kir – Mistari yote ya Biblia kuhusu Kir

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kir

2 Wafalme 16 : 9
9 ⑤ Na huyo mfalme wa Ashuru akamsikia; mfalme wa Ashuru akapanda juu ya Dameski, akautwaa, akawahamisha watu wake mateka mpaka Kiri, akamwua Resini.

Isaya 22 : 6
6 Na Elamu wameshika podo, pamoja na magari ya vita, na watu wenye kupanda farasi; na Kiri wameifunua ngao.

Amosi 1 : 5
5 Nami nitalivunja komeo la Dameski, na kuwakatilia mbali wenyeji wa bondeni mwa Aveni, na yeye aishikaye fimbo ya enzi katika Beth-Adini; na watu wa Shamu watakwenda uhamishoni hadi Kiri, asema BWANA.

Amosi 9 : 7
7 ③ Je! Ninyi si kama wana wa Wakushi kwangu mimi, enyi wana wa Israeli, asema BWANA? Je! Mimi sikuwapandisha Israeli toka nchi ya Misri, na Wafilisti toka Kaftori, na Washami toka Kiri?

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *