Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kilimo
Mathayo 13 : 1 – 10
1 Siku ile Yesu akatoka nyumbani, akaketi kando ya bahari.
2 Wakamkusanyikia makutano mengi, hata akapanda katika mashua, akaketi; na ule mkutano wote wakasimama pwani.
3 Akawaambia mambo mengi kwa mifano, akisema, Tazama, mpanzi alitoka kwenda kupanda.
4 Na alipokuwa akipanda, mbegu nyingine zilianguka karibu na njia, ndege wakaja wakazila;
5 nyingine zikaanguka penye miamba, pasipokuwa na udongo mwingi; zikaota haraka, kwa kukosa udongo wenye kina;
6 Lakini jua lilipozuka ziliungua; na kwa kuwa hazina mizizi zikanyauka.
7 Nyingine zikaanguka penye miiba; ile miiba ikamea, ikazisonga;
8 nyingine zikaanguka penye udongo mzuri, zikazaa, moja mia, moja sitini, moja thelathini.
9 Mwenye masikio na asikie.
10 Wakaja wanafunzi, wakamwambia, Kwa nini wasema nao kwa mifano?
1 Wakorintho 3 : 6 – 9
6 ⑰ Mimi nilipanda, Apolo akatia maji; bali mwenye kukuza ni Mungu.
7 Hivyo, apandaye si kitu, wala atiaye maji, bali Mungu akuzaye.
8 Basi yeye apandaye, na yeye atiaye maji ni wamoja, lakini kila mtu atapata thawabu yake mwenyewe kulingana na taabu yake mwenyewe.
9 ⑱ Maana sisi tu wafanya kazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu, ni jengo la Mungu.
Mwanzo 1 : 12
12 Nchi ikatoa majani, mche utoao mbegu kwa jinsi yake, na mti uzaao matunda, ambao mbegu zake zimo ndani yake, kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema.
Hosea 10 : 12
12 Jipandieni katika haki, vuneni kwa fadhili; uchimbueni udongo wa mashamba yenu, kwa maana wakati umewadia wa kumtafuta BWANA, hata atakapokuja na kuwanyeshea haki.
Leave a Reply