Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kigaga
Mambo ya Walawi 13 : 2
2 Mtu atakapokuwa na uvimbe katika ngozi ya mwili wake, au upele, au kipaku king’aacho, nao ukawa ni ugonjwa wa ukoma katika ngozi ya mwili wake, ndipo atakapoletwa kwa Haruni kuhani, au kwa mmojawapo wa wanawe makuhani;
Mambo ya Walawi 13 : 8
8 naye kuhani ataangalia, ikiwa huo upele umeenea katika ngozi, ndipo kuhani atasema kuwa ni najisi; ni ukoma.
Mambo ya Walawi 14 : 56
56 na kivimbe, na kikoko na kipaku king’aacho;
Mambo ya Walawi 21 : 20
20 au aliye na kibyongo, au aliyedumaa, au aliye na kilema cha jichoni, au aliye na upele, au mwenye buba, au aliyevunjika mapumbu;
Mambo ya Walawi 22 : 22
22 Kipofu, au aliyevunjika mahali, au kiwete au aliye na vidonda, au aliye na upele, au aliye na upele, hamtamtolea BWANA wanyama hao, wala msiwasongeze kwa BWANA kwa njia ya moto juu ya madhabahu.
Kumbukumbu la Torati 28 : 27
27 BWANA atakupiga kwa majipu ya Misri, na kwa bawasiri, na kwa pele, na kwa kujikuna, ambayo hupati kupoa.
Leave a Reply