Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kifo
Mwanzo 25 : 8
8 ⑭ Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.
Mwanzo 35 : 29
29 Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.
Maombolezo 1 : 19
19 Niliwaita hao walionipenda Lakini walinidanganya; Makuhani wangu na wazee wangu Walifariki mjini; Hapo walipokuwa wakitafuta chakula ili kuzihuisha nafsi zao.
Matendo 5 : 10
10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.
Ayubu 18 : 14
14 Atang’olewa katika hema yake aliyokuwa akiitumaini; Naye atapelekwa kwake mfalme wa vitisho.
Ayubu 14 : 14
14 Mtu akifa, je! Atakuwa hai tena? Mimi ningengoja siku zote za huduma yangu, Hadi kufunguliwa kwangu kunifikie.
Mwanzo 15 : 15
15 Lakini wewe utakwenda kwa baba zako kwa amani, utazikwa katika uzee mwema.
Mwanzo 25 : 8
8 ⑭ Abrahamu akafariki, naye akafa katika uzee mwema, mzee sana, ameshiba siku, akakusanyika kwa watu wake.
Mwanzo 35 : 29
29 Naye Isaka akakata roho, akafa, akakusanyika kwa watu wake, ni mzee, ameshiba siku. Esau na Yakobo, wanawe, wakamzika.
2 Petro 1 : 14
14 Nikijua kwamba kule kuwekea mbali maskani yangu kwaja upesi, kama Bwana wetu Yesu Kristo alivyonionesha.
Luka 12 : 20
20 Lakini Mungu akamwambia, Mpumbavu wewe, usiku huu wa leo wanataka roho yako! Na vitu ulivyojiwekea tayari vitakuwa vya nani?
Ayubu 16 : 22
22 Kwani ikiisha pita miaka michache, Nitakwenda njia hiyo ambayo sitarudi tena.
Mwanzo 49 : 33
33 Basi Yakobo alipokwisha kuwaagiza wanawe, akakunja miguu yake kitandani, akafa, akakusanywa pamoja na watu wake.
Zaburi 115 : 17
17 Wafu hawamsifu Mungu BWANA, Wala yeyote ashukaye kwenye kimya;
Mwanzo 3 : 19
19 kwa jasho la uso wako utakula chakula, hata utakapoirudia ardhi, ambayo katika hiyo ulitwaliwa; kwa maana u mavumbi wewe, nawe mavumbini utarudi.
Zaburi 104 : 29
29 Wewe wauficha uso wako, Wao wanafadhaika; Waiondoa pumzi yao, wanakufa, Na kuyarudia mavumbi yao,
Ayubu 14 : 2
2 Yeye huchanua kama vile ua, kisha hukatwa; Hukimbia kama kivuli, wala hakai kamwe.
Leave a Reply