Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kiapo
Mwanzo 14 : 23
23 ya kuwa sitatwaa uzi wala gidamu ya kiatu wala chochote kilicho chako, usije ukasema, Nimemtajirisha Abramu;
Mwanzo 21 : 23
23 ⑲ Basi sasa uniapie kwa Mungu, ya kuwa hutanitenda hila, wala mwanangu, wala mjukuu wangu, lakini kwa kadiri ya fadhili niliyokutendea utanitendea mimi, na nchi hii ambayo umetembea ndani yake.
Mwanzo 26 : 29
29 ⑧ ya kuwa hutatutenda mabaya, iwapo sisi hatukukugusa wewe, wala hatukukutendea ila mema, tukakuacha uende zako kwa amani; nawe sasa u mbarikiwa wa BWANA.
Mwanzo 26 : 31
31 ⑪ Wakaondoka asubuhi na mapema, wakaapiana wao kwa wao, kisha Isaka akawapa ruhusa, nao wakaenda zao kwa amani.
Mwanzo 24 : 3
3 ⑪ nami nitakuapisha kwa BWANA, Mungu wa mbingu, na Mungu wa nchi, kwamba hutamtwalia mwanangu mke katika binti za Wakanaani ambao nakaa kati yao;
Mwanzo 24 : 9
9 Yule mtumishi akaweka mkono wake chini ya paja la Abrahamu bwana wake, akamwapia katika neno hilo.
Mwanzo 25 : 33
33 Yakobo akamwambia, Niapie kwanza. Naye akamwapia, akamwuzia Yakobo haki yake ya mzaliwa wa kwanza.
Mwanzo 31 : 53
53 Mungu wa Abrahamu, na Mungu wa Nahori, Mungu wa baba yao, ahukumu kati yetu. Yakobo akaapa kwa Hofu ya Isaka baba yake.
Mwanzo 47 : 31
31 ⑰ Akanena, Niapie. Naye akamwapia. Israeli akajiinamisha kwenye mchago wa kitanda.
Mwanzo 50 : 25
25 Yusufu akawaapisha wana wa Israeli, akasema, Bila shaka Mungu atawajia ninyi, nanyi mtaipandisha huko mifupa yangu.
Yoshua 2 : 14
14 Wale wanaume wakamwambia, Tutautoa uhai wetu badala ya uhai wenu, ikiwa hamwitangazi habari ya shughuli yetu hii; kisha itakuwa, wakati BWANA atakapotupa nchi hii, tutakutendea kwa hisani na uaminifu.
Yoshua 6 : 22
22 ⑦ Naye Yoshua akawaambia wale wanaume wawili walioipeleleza nchi, Ingieni katika nyumba ya yule kahaba, mkamtoe huyo mwanamke mwenyewe na vitu vyote alivyo navyo, kama mlivyomwapia.
Leave a Reply