Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kazi
Tito 3 : 14
14 ⑩ Watu wetu nao wajifunze kudumu katika matendo mema, kwa matumizi yaliyo lazima, ili wasiwe hawana matunda.
Mathayo 5 : 16
16 ⑥ Vivyo hivyo nuru yenu na iangaze mbele ya watu, wapate kuyaona matendo yenu mema, wamtukuze Baba yenu aliye mbinguni.
Waraka kwa Waebrania 6 : 10
10 Maana Mungu si dhalimu hata aisahau kazi yenu, na pendo lile mlilolidhihirisha kwa jina lake, kwa kuwa mmewahudumia watakatifu, na hata hivi sasa mngali mkiwahudumia.
Yakobo 2 : 14 – 20
14 ① Ndugu zangu, yafaa nini, mtu akisema ya kwamba anayo imani, lakini hana matendo? Je! Ile imani yaweza kumwokoa?
15 Ikiwa ndugu mwanamume au ndugu mwanamke yu uchi na kupungukiwa na riziki,
16 ② na mmoja wenu akawaambia, Nendeni zenu kwa amani, mkaote moto na kushiba, lakini asiwape mahitaji ya kimwili, yafaa nini?
17 Vivyo hivyo na imani, isipokuwa ina matendo, imekufa nafsini mwake.
18 ③ Lakini mtu atasema, Wewe unayo imani, nami ninayo matendo. Nionyshe imani yako pasipo matendo, nami nitakuonesha imani yangu kwa njia ya matendo yangu.
19 ④ Wewe waamini ya kuwa Mungu ni mmoja; watenda vema. Mashetani nao waamini na kutetemeka.
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
Waefeso 2 : 8 – 10
8 ③ Kwa maana mmeokolewa kwa neema, kwa njia ya imani; ambayo hiyo haikutokana na nafsi zenu, ni kipawa cha Mungu;
9 ④ wala si kwa matendo, mtu awaye yote asije akajisifu.
10 ⑤ Maana tu kazi yake, tuliumbwa katika Kristo Yesu, tutende matendo mema, ambayo tokea awali Mungu aliyatengeneza ili tuenende nayo.
Tito 3 : 8
8 Ni neno la kuaminiwa; na mambo hayo nataka uyasisitizie sana, ili wale waliomwamini Mungu wakumbuke kudumu katika matendo mema. Mambo hayo ni mazuri sana, tena yana manufaa kwa wanadamu.
Yakobo 2 : 20 – 24
20 Lakini wataka kujua, wewe mwanadamu usiye kitu, kwamba imani pasipo matendo haizai?
21 ⑤ Je! Baba yetu Abrahamu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?
22 ⑥ Waona kwamba imani ilitenda kazi pamoja na matendo yake, na ya kwamba imani ile ilikamilishwa kwa njia ya matendo yale.
23 ⑦ Maandiko yale yakatimizwa yaliyonena, Abrahamu alimwamini Mungu, ikahesabiwa kwake kuwa ni haki; naye aliitwa rafiki wa Mungu.
24 ⑧ Mwaona kwamba mwanadamu huhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo yake; si kwa imani peke yake.
Tito 2 : 7
7 katika mambo yote ukijionesha wewe mwenyewe kuwa kielelezo cha matendo mema, na katika mafundisho yako ukionesha usahihi na ustahivu,
Yohana 15 : 14
14 Ninyi mmekuwa rafiki zangu, mkitenda niwaamuruyo.
Waraka kwa Waebrania 13 : 21
21 awafanye ninyi kuwa wakamilifu katika kila tendo jema, mpate kuyafanya mapenzi yake, naye akifanya ndani yetu lipendezalo mbele zake, kwa Yesu Kristo; utukufu una yeye milele na milele. Amina.
Leave a Reply