Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kawaida
Hesabu 1 : 52
52 Na wana wa Israeli watazipanga hema zao, kila mtu katika kambi yake mwenyewe, kila mtu hapo ilipo bendera yake mwenyewe, kama majeshi yao yalivyo.
Hesabu 2 : 2
2 Wana wa Israeli watapanga kila mtu penye bendera yake mwenyewe, na alama za nyumba za baba zao; kuikabili hema ya kukutania ndiko watakakopanga kwa kuizunguka pande zote.
Zaburi 20 : 5
5 Na tuushangilie wokovu wako, Kwa jina la Mungu wetu tuzitweke bendera zetu. BWANA akutimizie matakwa yako yote.
Wimbo ulio Bora 6 : 4
4 ⑰ Mpenzi wangu, u mzuri kama Tirza, Mwenye kupendeza kama Yerusalemu, Wa kutisha kama jeshi lenye bendera.
Wimbo ulio Bora 6 : 10
10 Ni nani huyu atazamaye kama alfajiri, Mzuri kama mwezi, safi kama jua, Wa kutisha kama wenye bendera?
Yeremia 4 : 21
21 Niione bendera hata lini, na kuisikia sauti ya tarumbeta?
Yeremia 4 : 6
6 Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamizi makuu.
Yeremia 50 : 2
2 ⑦ Tangazeni katika mataifa, Mkahubiri na kutweka bendera; Hubirini, msifiche, semeni, Babeli umetwaliwa! Beli amefedheheka; Merodaki amefadhaika; Sanamu zake zimeaibishwa, Vinyago vyake vimefadhaika.
Isaya 49 : 22
22 Bwana MUNGU asema hivi, Tazama, nitawainulia mataifa mkono wangu, na kuwainulia makabila ya watu bendera yangu; nao wataleta wana wako vifuani mwao, na binti zako watachukuliwa mabegani mwao.
Isaya 62 : 10
10 Piteni, piteni, katika malango; Itengenezeni njia ya watu; Tutieni, tutieni barabara; toeni mawe yake; Twekeni bendera kwa ajili ya makabila ya watu.
Yeremia 4 : 6
6 Twekeni bendera kuelekea Sayuni; kimbieni mpate kuwa salama, msikawie; kwa maana nitaleta mabaya toka kaskazini, na maangamizi makuu.
Leave a Reply