Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia kati
Mambo ya Walawi 19 : 31
31 Msiwaendee wenye pepo, wala wachawi; msiwatafute; ili kutiwa unajisi na wao; Mimi ndimi BWANA, Mungu wenu.
Mambo ya Walawi 20 : 27
27 ⑭ Tena mwanamume au mwanamke aliye na pepo, au aliye mchawi, hakika atauawa; watawapiga kwa mawe; damu yao itakuwa juu yao.
Isaya 8 : 19
19 ③ Na wakati watakapokuambia, Tafuta habari kwa watu wenye pepo na kwa wachawi; waliao kama ndege na kunong’ona; je! Haiwapasi watu kutafuta habari kwa Mungu wao? Je! Waende kwa watu waliokufa kwa ajili ya watu walio hai?
1 Mambo ya Nyakati 10 : 13 – 14
13 ① Basi Sauli alikufa kwa sababu ya kosa lake alilomkosa BWANA, kwa sababu ya neno la BWANA, asilolishika; na tena kwa kutaka shauri kwa mwenye pepo wa utambuzi, aulize kwake,
14 ② asiulize kwa BWANA; kwa hiyo akamwua, na ufalme akampa Daudi, mwana wa Yese.
Leave a Reply