Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kalamu
Waamuzi 5 : 14
14 ⑩ Kutoka Efraimu waliteremka wao ambao shina lao ni katika Amaleki, Nyuma yako, Benyamini, kati ya watu wako. Kutoka Makiri walishuka makamanda, Na kutoka Zabuloni wao washikao fimbo ya mwandishi.
Zaburi 45 : 1
1 Moyo wangu umefurika kwa jambo jema, Mimi nasema niliyomfanyia mfalme; Ulimi wangu ni kama kalamu ya mwandishi stadi.
Isaya 8 : 1
1 BWANA akaniambia, Ujipatie ubao mkubwa ukaandike juu yake kwa hati ya kawaida, Kwa Maher-shalal-hash-bazi;[2]
Yeremia 8 : 8
8 Mwasemaje, Sisi tuna akili, na Torati ya BWANA tunayo pamoja nasi? Lakini, tazama, kalamu yenye uongo ya waandishi imeifanya kuwa uongo.
3 Yohana 1 : 13
13 Nilikuwa na mambo mengi ya kukuandikia, lakini sipendi kukuandikia kwa wino na kalamu.
Ayubu 19 : 24
24 Yakachorwa katika mwamba milele, Kwa kalamu ya chuma na risasi.
Yeremia 17 : 1
1 Dhambi ya Yuda imeandikwa kwa kalamu ya chuma, na kwa ncha ya almasi; imechorwa katika kibao cha moyo wao, na katika pembe za madhabahu zenu;
Leave a Reply