Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Kadeshi
Yoshua 15 : 3
3 nao ukaendelea upande wa kusini wa kukwea kwenda Akrabimu, kisha ukaendelea hadi Sini, kisha ukaenda upande wa kusini wa Kadesh-barnea, kisha ukaendelea karibu na Hesroni, kisha ukafika Adari, na kuzunguka kwendea Karka;
Mwanzo 14 : 7
7 ⑱ Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Mwanzo 20 : 1
1 Abrahamu akaondoka huko kwenda nchi ya kusini, akakaa kati ya Kadeshi na Shuri, naye akatembea katika Gerari.
Mwanzo 14 : 7
7 ⑱ Kisha wakarudi wakaja mpaka Enmisfati, ndio Kadeshi, wakapiga nchi yote ya Waamaleki, na Waamori waliokaa Hasason-tamari.
Mwanzo 16 : 14
14 Kwa hiyo kisima kile kiliitwa Beer-lahai-roi.[4] Tazama, kiko kati ya Kadeshi na Beredi.
Hesabu 12 : 16
16 Baada ya hayo watu wakasafiri kutoka Haserothi, wakapiga kambi katika nyika ya Parani.
Hesabu 13 : 26
26 Wakaenda wakafika kwa Musa, na kwa Haruni, na kwa mkutano wote wa wana wa Israeli, katika jangwa la Parani, huko Kadeshi; wakawaletea habari, wao na mkutano wote, wakawaonesha matunda ya nchi.
Hesabu 20 : 1
1 ⑯ Kisha wana wa Israeli, mkutano wote, wakaingia jangwa la Sinai, katika mwezi wa kwanza, watu wakakaa Kadeshi; Miriamu akafa huko, akazikwa huko.
Hesabu 33 : 36
36 Wakasafiri kutoka Esion-geberi, wakapiga kambi katika nyika ya Sini (ni Kadeshi).
Yoshua 10 : 41
41 ④ Yoshua akawapiga kutoka Kadesh-barnea mpaka Gaza, na nchi yote ya Gosheni, hata Gibeoni.
Leave a Reply