Biblia inasema nini kuhusu jua – Mistari yote ya Biblia kuhusu jua

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia jua

Mhubiri 1 : 5
5 Jua lachomoza, na jua lashuka, na kufanya haraka kwenda mahali pa maawio yake.

Mwanzo 1 : 16
16 Mungu akaumba mianga miwili mikubwa, ule mkubwa utawale mchana, na ule mdogo utawale usiku; akafanya na nyota pia.

Ufunuo 22 : 5
5 Wala hapatakuwa na usiku tena; wala hawana haja ya taa wala ya nuru ya jua; kwa kuwa Bwana Mungu huwatia nuru, nao watatawala hata milele na milele.

Mwanzo 1 : 14
14 Mungu akasema, Na iwe mianga katika anga la mbingu ili itenge kati ya mchana na usiku; nayo iwe ndiyo dalili ya kuonesha majira, siku na miaka;

Ayubu 9 : 7
7 Aliamuruye jua, nalo halichomozi; Nazo nyota huzipiga mhuri.

Ezekieli 32 : 7
7 Nami nitakapokuzimisha, nitazifunika mbingu, na kuzifanya nyota zake kuwa giza; nami nitalifunika jua kwa wingu, wala mwezi hautatoa nuru yake.

Zaburi 19 : 4 – 6
4 Sauti yao imeenea duniani kote, Na maneno yao hadi miisho ya ulimwengu. Katika hizo ameliwekea jua hema,
5 Nalo hutokeza kama bwana arusi akitoka chumbani mwake, Lafurahi kama mtu aliye hodari Kwenda mbio katika njia yake.
6 Kuchomoza kwake ni katika mwisho wa mbingu, Na kuzunguka kwake ni hadi miisho ya mbingu, Wala hakuna kitu Kisichofikiwa na joto lake.

Ufunuo 16 : 8 – 9
8 Na huyo wa nne akalimimina bakuli lake juu ya jua, nalo likaruhusiwa kuwaunguza wanadamu kwa moto.
9 ② Wanadamu wakaunguzwa na joto kali, nao wakalitukana jina la Mungu aliye na mamlaka juu ya mapigo hayo; wala hawakutubu wala kumpa utukufu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *