Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Jose
Mathayo 13 : 55
55 Huyu si mwana wa seremala? Mamaye si yeye aitwaye Mariamu? Na nduguze si Yakobo, na Yusufu, na Simoni, na Yuda?
Mathayo 27 : 56
56 ⑯ Miongoni mwao alikuwamo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo na Yusufu, na mama yao wana wa Zebedayo.
Marko 6 : 3
3 Huyu si yule seremala, mwana wa Mariamu, na ndugu yao Yakobo, na Yose, na Yuda, na Simoni? Na dada zake hawapo hapa petu? Wakajikwaa kwake.
Marko 15 : 40
40 Palikuwako na wanawake wakitazama kwa mbali; miongoni mwao alikuwemo Mariamu Magdalene, na Mariamu mama yao Yakobo mdogo na Yose, na Salome;
Marko 15 : 47
47 Nao Mariamu Magdalene na Mariamu mamaye Yose wakapatazama mahali alipowekwa.
Matendo 4 : 36
36 ⑯ Na Yusufu, aliyeitwa na mitume Barnaba, (maana yake, Mwana wa faraja), Mlawi, asili yake ni mtu wa Kipro,
Leave a Reply