Biblia inasema nini kuhusu Jogoo Kuwika – Mistari yote ya Biblia kuhusu Jogoo Kuwika

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Jogoo Kuwika

Mathayo 26 : 34
34 ⑪ Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, usiku huu kabla ya kuwika jogoo, utanikana mara tatu.

Mathayo 26 : 75
75 Petro akalikumbuka lile neno la Yesu alilolisema, Kabla ya jogoo kuwika, utanikana mara tatu. Akatoka nje, akalia kwa majonzi.

Marko 13 : 35
35 Kesheni basi, kwa maana hamjui ajapo bwana wa nyumba, kwamba ni jioni, au kwamba ni usiku wa manane, au awikapo jogoo, au asubuhi;

Marko 14 : 30
30 ⑧ Yesu akamwambia, Amin, nakuambia wewe, Leo, usiku huu, kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu.

Marko 14 : 68
68 Akakana, akasema, Sijui wala sisikii unayoyasema wewe. Akatoka nje hadi ukumbini; jogoo akawika.

Marko 14 : 72
72 Na mara jogoo akawika mara ya pili. Petro akalikumbuka lile neno aliloambiwa na Yesu, Kabla ya kuwika jogoo mara mbili, utanikana mara tatu. Na alipolifikiri, akalia.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *