Biblia inasema nini kuhusu Jina – Mistari yote ya Biblia kuhusu Jina

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Jina

Mithali 22 : 1
1 Heri kuchagua jina jema kuliko mali nyingi; Na neema kuliko fedha na dhahabu.

Mhubiri 7 : 1
1 Heri sifa njema kuliko manukato ya thamani; Na siku ya kufa kuliko siku ya kuzaliwa.

Isaya 62 : 2
2 Na mataifa wataiona haki yako, na wafalme wote watauona utukufu wako; nawe utaitwa jina jipya, litakalotajwa na kinywa cha BWANA.

Mwanzo 17 : 5
5 ⑩ wala jina lako hutaitwa tena Abramu, lakini jina lako litakuwa Abrahamu,[5] kwani nimekuweka uwe baba wa mataifa mengi.

Mwanzo 17 : 15
15 Mungu akamwambia Abrahamu, Sarai mkeo, hutamwita jina lake Sarai, kwa kuwa jina lake litakuwa Sara.

Mwanzo 32 : 28
28 ⑱ Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, ila Israeli, maana umeshindana na Mungu, na watu, nawe umeshinda.

Hosea 1 : 4
4 BWANA akamwambia, Mwite jina lake Yezreeli; kwa maana bado kitambo kidogo, nitaipatiliza nyumba ya Yehu damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa nyumba ya Israeli.

Hosea 1 : 6
6 Akachukua mimba tena, akazaa mtoto wa kike, BWANA akamwambia, Mwite jina lake Lo-ruhama;[1] kwa maana sitairehemu nyumba ya Israeli tena, nisije nikawasamehe kwa njia yoyote.

Hosea 1 : 9
9 BWANA akasema, Mwite jina lake Lo-ami;[2] kwa maana ninyi si watu wangu, wala mimi sitakuwa Mungu wenu.

Hosea 2 : 1
1 Waambieni ndugu zenu, Ami[3] na dada zenu, Ruhama.[4]

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *