Biblia inasema nini kuhusu jicho kwa jicho โ€“ Mistari yote ya Biblia kuhusu jicho kwa jicho

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia jicho kwa jicho

Mathayo 5 : 38 โ€“ 39
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;
39 Lakini mimi nawaambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akupigaye shavu la kulia, mgeuzie na la pili.

Kutoka 21 : 24
24 โ‘ค jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu,

Warumi 12 : 17 โ€“ 19
17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.

Mathayo 5 : 38
38 Mmesikia kwamba imenenwa, Jicho kwa jicho, na jino kwa jino;

Mithali 13 : 3
3 โ‘ช Yeye alindaye kinywa chake huilinda nafsi yake; Bali afunuaye midomo yake atapata uharibifu.

1 Wathesalonike 5 : 15
15 Angalieni mtu awaye yote asimlipe mwenziwe mabaya kwa mabaya; bali siku zote lifuateni lililo jema, ninyi kwa ninyi na kwa watu wote.

Warumi 12 : 10 โ€“ 21
10 Kwa pendo la udugu, mpendane ninyi kwa ninyi; kwa heshima mkiwatanguliza wenzenu;
11 kwa bidii, bila kulegea; mkiwa na juhudi katika roho zenu; mkimtumikia Bwana;
12 kwa tumaini, mkifurahi; katika dhiki, mkisubiri; mkidumu katika kusali;
13 kwa mahitaji ya watakatifu, mkifuata ukarimu; katika kukaribisha wageni mkijitahidi.
14 Wabarikini wanaowaudhi; barikini, wala msilaani.
15 Furahini pamoja nao wafurahio; lieni pamoja nao waliao.
16 Mpatane nia zenu ninyi kwa ninyi. Msinuie yaliyo makuu, lakini mkubali kushughulishwa na mambo manyonge. Msiwe watu wa kujivunia akili.
17 Msimlipe mtu ovu kwa ovu. Angalieni yaliyo mema machoni pa watu wote.
18 Ikiwezekana, kwa upande wenu, mkae katika amani na watu wote.
19 Wapenzi, msijilipize kisasi, bali ipisheni ghadhabu ya Mungu; maana imeandikwa, Kisasi ni juu yangu mimi; mimi nitalipa, anena Bwana.
20 Lakini, Adui yako akiwa na njaa, mlishe; akiwa na kiu, mnyweshe; maana ufanyapo hivyo, utampalia makaa ya moto kichwani pake.
21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *