Biblia inasema nini kuhusu jela – Mistari yote ya Biblia kuhusu jela

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia jela

Isaya 61 : 1
1 Roho ya Bwana MUNGU i juu yangu; kwa sababu BWANA amenitia mafuta niwahubirie wanyenyekevu habari njema; amenituma ili kuwatibu waliovunjika moyo, kuwatangazia mateka uhuru wao, na hao waliofungwa habari za kufunguliwa kwao.

Ezra 7 : 26
26 Na kila mtu asiyekubali kuitenda sheria ya Mungu wako, na sheria ya mfalme, na apatilizwe hukumu kali, iwe ni kuuawa, au ni kuhamishwa, au kunyang’anywa mali yake, au kufungwa.

Mambo ya Walawi 24 : 12
12 Nao wakamtia kifungoni, ili wapate kuambiwa neno litakalotoka kinywani pa BWANA.

2 Timotheo 2 : 9
9 Nami katika hiyo nimeteswa hata kufungwa kama mtenda mabaya; lakini neno la Mungu halifungwi.

Mathayo 25 : 36
36 nilikuwa uchi, mkanivika nilikuwa mgonjwa, mkaja kunitazama; nilikuwa kifungoni, mkanijia.

Matendo 12 : 5
5 Basi Petro akalindwa gerezani, nalo kanisa likamwomba Mungu kwa juhudi kwa ajili yake.

Isaya 40 : 28 – 31
28 Je! Wewe hukujua? Hukusikia? Yeye Mungu wa milele, BWANA, Muumba miisho ya dunia, hazimii, wala hachoki; akili zake hazichunguziki.
29 Huwapa nguvu wazimiao, humwongezea nguvu yeye asiyekuwa na uwezo.
30 Hata vijana watazimia na kuchoka, na vijana wanaume wataanguka;
31 bali wao wamngojeao BWANA watapata nguvu mpya; watapanda juu kwa mbawa kama tai; watakimbia, wala hawatachoka; watakwenda kwa miguu, wala hawatazimia.

Warumi 14 : 1 – 23
1 ⑪ Yeye aliye dhaifu wa imani, mkaribisheni, lakini msimhukumu mawazo yake.
2 ⑫ Mtu mmoja anayo imani, anakula vyote; lakini yeye aliye dhaifu hula mboga.
3 ⑬ Yeye alaye asimdharau huyo asiyekula, wala yeye asiyekula asimhukumu huyo alaye; kwa maana Mungu amemkubali.
4 ⑭ Wewe u nani unayemhukumu mtumishi wa mwingine? Kwa bwana wake mwenyewe yeye husimama au huanguka. Naam, atasimamishwa, kwa kuwa Bwana aweza kumsimamisha.
5 ⑮ Mtu mmoja afanya tofauti kati ya siku na siku, mwingine aona siku zote kuwa sawasawa. Kila mtu na athibitike katika akili zake mwenyewe.
6 Yeye aadhimishaye siku, huiadhimisha kwa Bwana; naye alaye, hula kwa Bwana, kwa maana amshukuru Mungu; tena asiyekula, hali kwa Bwana, naye pia amshukuru Mungu.
7 Kwa sababu hakuna mtu miongoni mwetu aishiye kwa nafsi yake, wala hakuna afaye kwa nafsi yake.
8 ⑯ Kwa maana kama tukiishi, twaishi kwa Bwana, au kama tukifa, twafa kwa Bwana. Basi kama tukiishi au kama tukifa, tu mali ya Bwana.
9 Maana Kristo alikufa akawa hai tena kwa sababu hii, awamiliki waliokufa na walio hai pia.
10 ⑰ Lakini wewe je! Mbona wamhukumu ndugu yako? Au wewe je! Mbona wamdharau ndugu yako? Kwa maana sisi sote tutasimama mbele ya kiti cha hukumu cha Mungu.
11 ⑱ Kwa kuwa imeandikwa, Kama niishivyo, anena Bwana, kila goti litapigwa mbele zangu; Na kila ulimi utamkiri Mungu.
12 ⑲ Basi ni hivyo, kila mtu miongoni mwetu atatoa habari zake mwenyewe mbele za Mungu.
13 Basi tusiendelee kuhukumiana, bali amueni kuwa mtu asifanye kitu cha kumkwaza ndugu au cha kumwangusha.
14 ⑳ Najua, tena nimehakikishwa sana katika Bwana Yesu, ya kuwa hakuna kitu kilicho najisi kwa asili yake, lakini kwake yeye akionaye kitu kuwa najisi, kwake huyo kitu kile ni najisi.
15 Na ndugu yako akichukizwa kwa sababu ya chakula, umeacha kwenda katika upendo. Kwa chakula chako usimharibu mtu yule ambaye Kristo alikufa kwa ajili yake.
16 Basi, huo wema wenu usitajwe kwa ubaya.
17 Maana ufalme wa Mungu si kula wala kunywa, bali ni haki na amani na furaha katika Roho Mtakatifu.
18 Kwa kuwa yeye amtumikiaye Kristo katika mambo hayo humpendeza Mungu, tena hukubaliwa na wanadamu.
19 Basi kama ni hivyo, na mfuate mambo ya amani na mambo yafaayo kwa kujengana.
20 Kwa ajili ya chakula usiiharibu kazi ya Mungu. Kweli, vyote ni safi; bali ni vibaya kwa mtu alaye na kujikwaza.
21 Ni vyema kutokula nyama wala kunywa divai wala kutenda neno lolote ambalo kwa hilo ndugu yako hukwazwa.
22 Ile imani uliyo nayo uwe nayo nafsini mwako mbele za Mungu. Heri mtu yule asiyejihukumu nafsi yake katika neno lile analolikubali.
23 Lakini aliye na mashaka, kama akila, amehukumiwa kuwa ana hatia, kwa maana hakula kwa imani. Na kila tendo lisilotoka katika imani ni dhambi.

Hesabu 15 : 34
34 Nao wakamweka kifungoni, maana, lilikuwa halijasemwa atakalotendwa.

Wafilipi 1 : 27
27 Lakini mwenendo wenu na uwe kama inavyoipasa Injili ya Kristo, ili, nikija na kuwaona ninyi, au nisipokuwapo, niyasikie mambo yenu, kama mnasimama imara katika roho moja, kwa moyo mmoja mkiishindania imani ya Injili;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *