Biblia inasema nini kuhusu Isaka – Mistari yote ya Biblia kuhusu Isaka

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Isaka

Mwanzo 17 : 19
19 ⑳ Mungu akasema, Sivyo, lakini Sara mkeo atakuzalia mwana wa kiume, nawe utamwita jina lake Isaka. Nami nitafanya agano langu imara kwake kuwa agano la milele kwa ajili ya uzao wake baada yake.

Mwanzo 18 : 15
15 Akakana Sara, akisema, Sikucheka, maana aliogopa. Naye akasema, Sivyo! Umecheka.

Mwanzo 21 : 8
8 Mtoto akakua, akaachishwa kunyonya; Abrahamu akafanya karamu kuu siku ile Isaka alipoachishwa kunyonya.

Yoshua 24 : 3
3 ② Nami nikamtwaa Abrahamu baba yenu toka ng’ambo ya Mto, nikamwongoza katika nchi yote ya Kanaani; nikaongeza uzao wake, nikampa Isaka.

1 Mambo ya Nyakati 1 : 28
28 Wana wa Abrahamu; Isaka, na Ishmaeli.

Wagalatia 4 : 28
28 Basi, ndugu zangu, kama Isaka sisi tu watoto wa ahadi.

Waraka kwa Waebrania 11 : 11
11 Kwa imani hata Sara mwenyewe alipokea uwezo wa kuwa na mimba; alipokuwa amepita wakati wake; kwa kuwa alimhesabu yeye aliyeahidi kuwa mwaminifu.

Mathayo 1 : 2
2 Abrahamu alimzaa Isaka; Isaka akamzaa Yakobo; Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake;

Mwanzo 22 : 19
19 Basi Abrahamu akawarudia vijana wake, wakaondoka, wakaenda zao pamoja mpaka Beer-sheba; Abrahamu akakaa huko Beer-sheba.

Waraka kwa Waebrania 11 : 17
17 Kwa imani Abrahamu alipojaribiwa, akamtoa Isaka awe dhabihu; na yeye aliyezipokea hizo ahadi alikuwa akimtoa mwanawe, mzaliwa pekee;

Yakobo 2 : 21
21 ⑤ Je! Baba yetu Abrahamu hakuhesabiwa kuwa ana haki kwa matendo, hapo alipomtoa Isaka mwanawe juu ya madhabahu?

Mwanzo 25 : 20
20 Isaka akawa mwenye miaka arubaini alipomtwaa Rebeka binti Bethueli, Mshami, wa Padan-aramu, ndugu wa Labani, Mshami, kuwa mke wake.

Mwanzo 26 : 5
5 Kwa sababu Abrahamu alisikia sauti yangu, akayahifadhi maagizo yangu, na amri zangu, na hukumu zangu, na sheria zangu.

1 Mambo ya Nyakati 16 : 19
19 Mlipokuwa watu wawezao kuhesabiwa; Naam, watu wachache na wageni ndani yake.

Mwanzo 24 : 62
62 ⑥ Basi Isaka alikuwa amekuja kwa njia ya Beer-lahai-roi, maana alikaa katika nchi ya kusini.

Mwanzo 25 : 11
11 ⑰ Ikawa, baada ya kufa kwake Abrahamu, Mungu akambariki Isaka mwanawe. Naye Isaka akakaa karibu ya Beer-lahai-roi.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *