Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia imba
Yakobo 5 : 13
13 Kuna mtu miongoni mwenu anayeteseka? Na aombe. Ana moyo wa kuchangamka? Na aimbe zaburi.
Zaburi 9 : 2
2 Nitafurahi na kukushangilia; Nitaliimbia sifa jina lako, Wewe Uliye juu.
Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.
Zaburi 100 : 1 – 2
1 Mshangilieni BWANA, enyi nchi zote;
2 Mtumikieni BWANA kwa furaha; Njoni mbele zake mkiimba;
Isaya 49 : 13
13 Imbeni, enyi mbingu; ufurahi, Ee nchi; Pazeni sauti ya kuimba, enyi milima; Kwa kuwa BWANA amewafariji watu wake, Naye atawahurumia watu wake walioteswa.
Leave a Reply