Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia imani
Yohana 16 : 7 – 11
7 ⑧ Lakini mimi nawaambia iliyo kweli; yawafaa ninyi mimi niondoke, kwa maana mimi nisipoondoka, huyo Msaidizi hatakuja kwenu; bali mimi nikienda zangu, nitamtuma kwenu.
8 ⑩ Naye akiisha kuja, huyo atauhakikisha ulimwengu kwa habari ya dhambi, na haki, na hukumu.
9 ⑪ Kwa habari ya dhambi, kwa sababu hawaniamini mimi;
10 ⑫ kwa habari ya haki, kwa sababu mimi naenda zangu kwa Baba, wala hamnioni tena;
11 ⑬ kwa habari ya hukumu, kwa sababu yule mkuu wa ulimwengu huu amekwisha kuhukumiwa.
Leave a Reply