Biblia inasema nini kuhusu Ibada – Mistari yote ya Biblia kuhusu Ibada

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Ibada

Kutoka 20 : 3
3 ⑮ Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Kumbukumbu la Torati 5 : 7
7 Usiwe na miungu mingine ila mimi.

Kumbukumbu la Torati 6 : 13
13 Mche BWANA, Mungu wako; ndiye utakayemtumikia, na kuapa kwa jina lake.

Mathayo 4 : 10
10 Ndipo Yesu alipomwambia, Nenda zako, Shetani; kwa maana imeandikwa, Mwabudu Bwana Mungu wako, na umtumikie yeye peke yake.

Luka 4 : 8
8 ⑳ Yesu akajibu akamwambia, Imeandikwa, Msujudie Bwana Mungu wako, umwabudu yeye peke yake.

Matendo 10 : 26
26 ⑤ Lakini Petro akamwinua, akasema, Simama, mimi nami ni mwanadamu.

Matendo 14 : 15
15 ⑤ wakisema, Akina bwana, mbona mnafanya haya? Sisi nasi tu wanadamu hali moja na ninyi; tunawahubiria Habari Njema, ili mgeuke na kuyaacha mambo haya ya ubatili na kumwelekea Mungu aliye hai, aliyeumba mbingu na nchi na bahari na vitu vyote vilivyomo;

Wakolosai 2 : 18
18 Mtu asiwanyang’anye thawabu yenu, kwa kunyenyekea kwa mapenzi yake mwenyewe tu, na kuabudu malaika, akijitia katika maono yake na kujivuna bure, kwa akili zake za kimwili;

Ufunuo 19 : 10
10 ⑳ Nami nikaanguka mbele ya miguu yake, ili nimsujudie; akaniambia, Angalia, usifanye hivi; mimi ni mtumishi mwenzako na wa ndugu zako walio na ushuhuda wa Yesu. Msujudie Mungu. Kwa maana ushuhuda wa Yesu ndio roho ya unabii.

Mwanzo 4 : 4
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. BWANA akamtakabali Habili na sadaka yake;

Mwanzo 8 : 21
21 BWANA akasikia harufu ya kumridhisha; BWANA akasema moyoni, Sitailaani nchi tena baada ya hayo kwa sababu ya wanadamu, maana mawazo ya moyo wa mwanadamu ni mabaya tangu ujana wake; wala sitapiga tena baada ya hayo kila kilicho hai kama nilivyofanya. 1

Mwanzo 4 : 5
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.

Kutoka 28 : 38
38 Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Haruni, na Haruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili vipate kukubaliwa mbele za BWANA.

Yeremia 26 : 2
2 ④ BWANA asema hivi, Simama katika uwanja wa nyumba ya BWANA, useme na miji yote ya Yuda, wajao ili kuabudu katika nyumba ya BWANA; sema nao maneno yote ninayokuamuru kuwaambia, usizuie hata neno moja.

Luka 18 : 10
10 Watu wawili walipanda kwenda hekaluni kusali, mmoja Farisayo, wa pili mtoza ushuru.

Luka 24 : 53
53 Nao daima walikuwa ndani ya hekalu, wakimsifu Mungu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *