Biblia inasema nini kuhusu Horebu – Mistari yote ya Biblia kuhusu Horebu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Horebu

Kutoka 3 : 1
1 ④ Basi huyo Musa alikuwa akilichunga kundi la Yethro mkwewe, kuhani wa Midiani; akaliongoza kundi nyuma ya jangwa, akafika mpaka mlima wa Mungu, hata Horebu.

Kutoka 17 : 6
6 Tazama, nitasimama mbele yako huko, juu ya lile jabali katika Horebu; nawe utalipiga jabali, na maji yatatoka, watu wapate kunywa. Musa akafanya hivyo mbele ya wazee wa Israeli.

Kutoka 33 : 6
6 Basi wana wa Israeli wakavua mapambo yao, tangu mlima wa Horebu na mbele.

Kumbukumbu la Torati 1 : 2
2 Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya mlima wa Seiri mpaka Kadesh-barnea.

Kumbukumbu la Torati 1 : 6
6 BWANA, Mungu wetu, alituambia huko Horebu, akasema, Mmekaa katika mlima huu vya kutosha;

Kumbukumbu la Torati 1 : 19
19 Tukasafiri kutoka Horebu, tukapita katikati ya jangwa lile kubwa la kutisha mliloliona, njia ile ya kuiendea nchi ya vilima vya Waamori, kama BWANA, Mungu wetu, alivyotuamuru, tukafika Kadesh-barnea.

Kumbukumbu la Torati 4 : 10
10 ⑪ siku ile uliyosimama mbele za BWANA wako huko Horebu, BWANA aliponiambia, Nikusanyieni watu hawa, nami nitawafanya wasikilize maneno yangu, ili wajifunze kunicha mimi siku zote watakazoishi duniani, wakapate na kuwafundisha watoto wao.

Kumbukumbu la Torati 4 : 15
15 ⑯ Jihadharini nafsi zenu basi; maana hamkuona umbo la namna yoyote siku ile BWANA aliyosema nanyi kutoka kati ya moto;

Kumbukumbu la Torati 5 : 2
2 BWANA, Mungu wetu, alifanya agano nasi katika Horebu.

Kumbukumbu la Torati 9 : 8
8 Tena mlimkasirisha BWANA katika Horebu, BWANA akakasirika hadi akataka kuwaangamiza.

Kumbukumbu la Torati 29 : 1
1 Haya ndiyo maneno ya agano BWANA alilomwamuru Musa alifanye na wana wa Israeli katika nchi ya Moabu, pamoja na agano alilofanya nao Horebu.

1 Wafalme 8 : 9
9 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili za mawe ambazo Musa aliziweka ndani huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka katika nchi ya Misri.

1 Wafalme 19 : 8
8 Akainuka, akala, akanywa, akaenda katika nguvu za chakula hicho siku arubaini mchana na usiku hata akafika Horebu, mlima wa Mungu.

2 Mambo ya Nyakati 5 : 10
10 Hamkuwa na kitu ndani ya sanduku, ila zile mbao mbili alizozitia Musa huko Horebu, BWANA alipofanya agano na wana wa Israeli, hapo walipotoka Misri.

Zaburi 106 : 19
19 Walifanya ndama huko Horebu, Wakaisujudia sanamu ya kusubu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *