Biblia inasema nini kuhusu Hophni – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hophni

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hophni

1 Samweli 1 : 3
3 Na mtu huyo alikuwa akikwea kutoka mjini kwake mwaka kwa mwaka, ili kuabudu, na kumtolea BWANA wa majeshi dhabihu katika Shilo. Na wale wana wawili wa Eli, Hofni na Finehasi, makuhani wa BWANA, walikuwako huko.

1 Samweli 2 : 36
36 ⑱ Kisha itakuwa, ya kwamba kila mtu atakayesalia katika nyumba yako atakwenda kumsujudia, apate kipande kidogo cha fedha, na mkate mmoja; na kumwambia, Tafadhali nitie katika kazi mojawapo ya ukuhani, nipate kula kipande kidogo cha mkate.

1 Samweli 3 : 14
14 Na kwa hiyo nimeapa juu ya nyumba ya Eli, ya kwamba uovu wa nyumba ya Eli hautasafika kwa dhabihu wala kwa sadaka hata milele.

1 Samweli 4 : 4
4 Basi wakatuma watu kwenda Shilo, nao wakalileta toka huko sanduku la Agano la BWANA wa majeshi, akaaye juu ya makerubi; na Hofni na Finehasi, wana wawili wa Eli, walikuwako huko pamoja na sanduku la Agano la Mungu.

1 Samweli 4 : 11
11 Hilo sanduku la Mungu likatwaliwa; na Hofni na Finehasi, wale wana wawili wa Eli, wakauawa.

1 Samweli 4 : 17
17 Yeye aliyeleta habari akajibu, akasema, Israeli wamekimbia mbele ya Wafilisti, tena watu wengi sana wameuawa, hata na wana wako wawili, Hofni na Finehasi, wamekufa pia, na sanduku la Mungu limetwaliwa.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *