Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Homa
Mambo ya Walawi 26 : 16
16 mimi nami nitawatenda jambo hili; nitaamrisha uje juu yenu utisho, hata kifua kikuu na homa, zitakazoharibu macho yenu, na kuidhoofisha roho; nanyi mtapanda mbegu yenu bure, kwa kuwa adui zenu wataila.
Kumbukumbu la Torati 28 : 22
22 BWANA atakupiga kwa kifua kikuu, na kwa homa, na kwa kuwashwa, na kwa joto jingi, na kwa upanga, na kwa ukaufu, na kwa koga; navyo vitakufukuza hata uangamie.
Ayubu 30 : 30
30 Ngozi yangu ni nyeusi, nayo yanitoka, Na mifupa yangu imeteketea kwa joto.
Zaburi 22 : 15
15 ⑫ Nguvu zangu zimekauka kama gae, Ulimi wangu waambatana na taya zangu; Unaniweka katika mavumbi ya mauti
Mathayo 8 : 14
14 Na Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, akamwona mkwe wa Petro, mamaye mkewe, amelala kitandani akiugua homa.
Matendo 28 : 8
8 Ikawa babake Publio alikuwa akiugua homa na kuhara damu. Paulo akaingia kwake, akaomba, akaweka mikono yake juu yake, na kumponya.
Leave a Reply