Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hofu ya Bwana
Mithali 8 : 13
13 Kumcha BWANA ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia.
Mithali 1 : 7
7 Kumcha BWANA ni chanzo cha maarifa, Bali wapumbavu hudharau hekima na adabu.
Mathayo 10 : 28
28 ⑤ Msiwaogope wauuao mwili, wasiweze kuiua na roho; afadhali mwogopeni yule awezaye kuangamiza mwili na roho pia katika Jehanamu.
Mhubiri 12 : 13
13 Hii ndiyo jumla ya maneno; yote yamekwisha sikiwa; Mche Mungu, nawe uzishike amri zake, Maana kwa jumla ndiyo impasayo mtu.
Zaburi 33 : 8
8 Nchi yote na imwogope BWANA, Wote wakaao duniani na wamche.
Mithali 14 : 26
26 Kumcha BWANA ni tumaini imara; Watoto wake watakuwa na kimbilio.
Ayubu 28 : 28
28 Kisha akamwambia mwanadamu, Tazama, kumcha Bwana ndiyo hekima, Na kujitenga na uovu ndio ufahamu.
Mithali 14 : 27
27 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.
Zaburi 25 : 14
14 Siri ya BWANA iko kwao wamchao, Naye atawajulisha agano lake.
Luka 1 : 50
50 Na rehema zake hudumu vizazi hata vizazi Kwa hao wanaomcha.
Mithali 3 : 7
7 ⑤ Usiwe na hekima machoni pako; Mche BWANA, ukajiepushe na uovu.
1 Yohana 4 : 18
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.
Kumbukumbu la Torati 10 : 12
12 ⑤ Na sasa, Israeli, BWANA, Mungu wako, anataka nini kwako, ila umche BWANA, Mungu wako, na kwenda katika njia zake zote, na kumpenda, na kumtumikia BWANA, Mungu wako, kwa moyo wako wote, na kwa roho yako yote;
Zaburi 111 : 10
10 ⑯ Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.
Zaburi 86 : 11
11 Ee BWANA, unifundishe njia yako; Nitakwenda katika kweli yako; Moyo wangu na ufurahi kulicha jina lako;
Isaya 41 : 10
10 ② usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.
Zaburi 19 : 9
9 Kicho cha BWANA ni kitakatifu, Kinadumu milele. Hukumu za BWANA ni kweli, Zina haki kabisa.
Waraka kwa Waebrania 10 : 26 – 31
26 ⑬ Maana, kama tukifanya dhambi kusudi baada ya kuupokea ujuzi wa ile kweli, haibaki tena dhabihu kwa ajili ya dhambi;
27 ⑭ bali kuna kuitazamia hukumu yenye kutisha, na ukali wa moto ulio tayari kuwala wao wapingao.
28 ⑮ Mtu aliyeidharau Sheria ya Musa hufa pasipo huruma, kwa neno la mashahidi wawili au watatu.
29 ⑯ Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema?
30 ⑰ Maana twamjua yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu yangu, mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake.
31 ⑱ Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.
Matendo 10 : 35
35 ⑦ bali katika kila taifa mtu amchaye na kutenda haki hukubaliwa na yeye.
Wafilipi 2 : 12 – 13
12 Basi, wapendwa wangu, kama vile mlivyotii sikuzote, si wakati mimi nilipokuwapo tu, bali sasa zaidi sana mimi nisipokuwapo, utimizeni wokovu wenu wenyewe kwa kuogopa na kutetemeka.
13 Kwa maana ndiye Mungu atendaye kazi ndani yenu, kutaka kwenu na kutenda kwenu, kwa kulitimiza kusudi lake jema.
Leave a Reply