Biblia inasema nini kuhusu hofu – Mistari yote ya Biblia kuhusu hofu

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hofu

2 Timotheo 1 : 7
7 Maana Mungu hakutupa roho ya woga, bali ya nguvu na ya upendo na ya moyo wa kiasi.

Isaya 41 : 10
10 ② usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kulia wa haki yangu.

1 Yohana 4 : 18
18 Katika pendo hamna hofu; lakini pendo lililo kamili huitupa nje hofu, kwa maana hofu ina adhabu; na mwenye hofu hakukamilishwa katika pendo.

Wafilipi 4 : 6
6 Msijisumbue kwa neno lolote; bali katika kila neno kwa kusali na kuomba, pamoja na kushukuru, haja zenu na zijulikane na Mungu.

Zaburi 111 : 10
10 ⑯ Kumcha BWANA ndio mwanzo wa hekima, Wote wafanyao hayo wana ufahamu mzuri, Sifa zake zadumu milele.

Mithali 19 : 23
23 ① Kumcha BWANA huelekea uhai; Atakaa ameshiba; hatajiliwa na ubaya.

Mithali 14 : 27
27 Kumcha BWANA ni chemchemi ya uzima, Ili kuepukana na tanzi za mauti.

Mithali 29 : 25
25 ⑯ Kuwaogopa wanadamu huleta mtego; Bali amtumainiye BWANA atakuwa salama.

Zaburi 34 : 4
4 ② Nilimtafuta BWANA, naye akanijibu, Akaniokoa kutoka kwa hofu zangu zote.

1 Yohana 1 : 9
9 Tukiziungama dhambi zetu, Yeye ni mwaminifu na wa haki hata atuondolee dhambi zetu, na kututakasa na udhalimu wote.

1 Petro 2 : 17
17 ⑮ Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu. Mcheni Mungu. Mpeni heshima mfalme.

Warumi 8 : 15
15 Kwa kuwa hamkupokea tena roho wa utumwa iletayo hofu; bali mlipokea roho ya kufanywa wana, ambayo kwa hiyo twalia, Aba, yaani, Baba.

Isaya 43 : 1 – 3
1 Lakini sasa, BWANA aliyekuhuluku, Ee Yakobo, yeye aliyekuumba, Ee Israeli, asema hivi, Usiogope, maana nimekukomboa; nimekuita kwa jina lako, wewe u wangu.
2 Upitapo katika maji mengi nitakuwa pamoja nawe; na katika mito, haitakugharikisha; uendapo katika moto, hutateketea; wala mwali wa moto hautakuunguza.
3 Maana mimi ni BWANA, Mungu wako; Mtakatifu wa Israeli, Mwokozi wako, nimetoa Misri kuwa ukombozi wako; nimetoa Kushi na Seba kwa ajili yako.

2 Wakorintho 5 : 17
17 Hata imekuwa, mtu akiwa ndani ya Kristo amekuwa kiumbe kipya; ya kale yamepita, tazama! Yamekuwa mapya.

2 Mambo ya Nyakati 17 : 10
10 ⑪ Hofu ya BWANA ikaziangukia falme za nchi zote zilizozunguka Yuda, wasipigane vita na Yehoshafati.

Matendo 9 : 31
31 Basi kanisa likapata raha kote katika Yudea na Galilaya na Samaria, likajengwa, likiendelea na kuongezeka katika kicho cha Bwana, na faraja ya Roho Mtakatifu.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *