Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hisia tano
Zaburi 34 : 8
8 ⑤ Onjeni muone ya kuwa BWANA yu mwema; Heri mtu yule anayemtumainia.
1 Yohana 1 : 1 – 4
1 Lile lililokuwako tangu mwanzo, tulilolisikia, tuliloliona kwa macho yetu, tulilolitazama, na mikono yetu ikalipapasa, kuhusu Neno la uzima;
2 (na uzima huo ulidhihirika, nasi tumeona, tena tunashuhudia, na kuwahubiria ninyi ule uzima wa milele, uliokuwa kwa Baba, ukadhihirika kwetu);
3 hilo tuliloliona na kulisikia, tunawahubiria na ninyi; ili nanyi pia mpate kushirikiana nasi: na ushirika wetu ni pamoja na Baba, na pamoja na Mwana wake Yesu Kristo.
4 Na haya tunayaandika, ili furaha yetu itimizwe.
Mithali 20 : 12
12 ⑧ Sikio lisikialo, na jicho lionalo, BWANA ndiye aliyeyafanya yote mawili.
Mathayo 5 : 13
13 ③ Ninyi ni chumvi ya dunia; lakini chumvi ikipoteza ladha yake, ladha hiyo itarudishwa vipi? Haifai tena kabisa, ila kutupwa nje na kukanyagwa na watu.
Zaburi 94 : 9
9 Aliyelitia sikio mahali pake, asisikie? Aliyelifanya jicho, asione?
Kutoka 20 : 8
8 ⑳ Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
Isaya 66 : 8
8 Ni nani aliyesikia neno kama hili? Ni nani aliyeona mambo kama haya? Je! Nchi yaweza kuzaliwa kwa siku moja? Taifa laweza kuzaliwa mara? Maana Sayuni, mara alipopata uchungu, Alizaa watoto wake.
Leave a Reply