Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hiram
2 Samweli 5 : 11
11 ④ Kisha Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na maseremala, na waashi; nao wakamjengea Daudi nyumba.
1 Mambo ya Nyakati 14 : 1
1 Naye Hiramu, mfalme wa Tiro, akatuma wajumbe kwa Daudi, akampelekea na mierezi, na waashi, na maseremala, ili wamjengee nyumba.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 3
3 Sulemani akatuma watu kwa Hiramu[2] mfalme wa Tiro, akisema, Kama ulivyomtendea baba yangu Daudi, na kumletea mierezi, ajijengee nyumba ya kukaa, unitendee na mimi.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 16
16 ① nasi tutakata miti katika Lebanoni, kadiri utakavyohitaji; na kukuletea tukiieleza baharini mpaka Yafa; nawe utaipeleka Yerusalemu.
1 Wafalme 9 : 13
13 Akasema, Miji gani hii uliyonipa, ndugu yangu? Akaiita nchi ya Kabuli,[18] hata leo.
1 Wafalme 9 : 14
14 Hiramu alikuwa amemletea mfalme talanta[19] mia moja na ishirini za dhahabu.
1 Wafalme 9 : 28
28 Wakafika Ofiri, wakachukua toka huko dhahabu, talanta[20] mia nne na ishirini, wakamletea mfalme Sulemani.
1 Wafalme 10 : 11
11 Tena merikebu za Hiramu, zilizochukua dhahabu kutoka Ofiri, zikaleta kutoka Ofiri miti ya msandali mingi sana, na vito vya thamani.
1 Wafalme 7 : 45
45 ⑯ na masufuria, na majembe, na mabeseni; hata vyombo hivyo vyote, Huramu alivyomfanyia mfalme Sulemani, katika nyumba ya BWANA, vyote vilikuwa vya shaba iliyosuguliwa.
2 Mambo ya Nyakati 2 : 13
13 Na sasa nimemtuma mtu stadi, mwenye akili, yaani, Hiramu[5] baba yangu,
2 Mambo ya Nyakati 4 : 16
16 Vyungu, pia sepetu, nyuma na vyombo vingine vyote, Huram-abi[16] akamtengenezea mfalme Sulemani kwa ajili ya nyumba ya BWANA, vilikuwa vya shaba iliyong’arishwa.
Leave a Reply