Biblia inasema nini kuhusu Herode – Mistari yote ya Biblia kuhusu Herode

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Herode

Luka 3 : 1
1 Mwaka wa kumi na tano wa kutawala kwake Kaisari Tiberio, Pontio Pilato alipokuwa mtawala wa Yudea, na Herode mfalme wa Galilaya, na Filipo, ndugu yake, mfalme wa Iturea na nchi ya Trakoniti, na Lisania mfalme wa Abilene,

Luka 23 : 7
7 Na alipopata habari ya kuwa yu chini ya mamlaka ya Herode, alimpeleka kwa Herode, kwa kuwa yeye naye alikuwapo Yerusalemu siku zile.

Mathayo 14 : 4
4 ⑲ Kwa sababu Yohana alimwambia, Si halali kwako kuwa naye.

Marko 6 : 19
19 Naye yule Herodia akawa akimvizia, akataka kumwua, asiweze.

Marko 6 : 28
28 akakileta kichwa chake katika kombe, akampa yule kijana, naye yule kijana akampa mamaye.

Luka 9 : 7
7 Na Herode mfalme akasikia habari za yote yaliyotendeka, akafadhaika kwa sababu watu wengine walisema ya kwamba Yohana amefufuka katika wafu,

Luka 9 : 9
9 Lakini Herode akasema, Yohana nilimkata kichwa; basi ni nani huyu ambaye ninasikia mambo haya juu yake? Akataka kumwona.

Luka 23 : 8
8 Herode alipomwona Yesu alifurahi sana, kwa sababu alikuwa akitaka sana kumwona tangu siku nyingi, maana amesikia habari zake, akatarajia kuona ishara iliyofanywa na yeye.

Luka 13 : 32
32 Akawaambia, Nendeni, mkamwambie yule mbweha, Tazama, leo na kesho natoa pepo na kuponya wagonjwa, siku ya tatu nakamilisha kazi yangu.

Luka 23 : 12
12 Basi siku ile ile Herode na Pilato walipatana kwa urafiki kwa maana hapo kwanza walikuwa na uadui wao kwa wao.

Luka 23 : 15
15 wala hata Herode, kwa maana amemrudisha kwetu; basi tazama, hakuna neno lolote alilolitenda lipasalo kufa.

Matendo 4 : 27
27 ⑧ Maana ni kweli, Herode na Pontio Pilato pamoja na Mataifa na watu wa Israeli, walikusanyika katika mji huu juu ya Mtumishi wako mtakatifu Yesu, uliyemtia mafuta,

Matendo 12 : 23
23 Mara malaika wa Bwana akampiga, kwa sababu hakumpa Mungu utukufu; akaliwa na wadudu, akatokwa na roho.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *