Biblia inasema nini kuhusu hekima – Mistari yote ya Biblia kuhusu hekima

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hekima

Yakobo 1 : 5
5 Lakini mmoja wenu akipungukiwa na hekima, na aombe dua kwa Mungu, awapaye wote, kwa ukarimu, wala hakemei; naye atapewa.

Waefeso 5 : 15 – 17
15 Basi angalieni sana jinsi mnavyoenda; si kama watu wasio na hekima bali kama watu wenye hekima;
16 mkiukomboa wakati kwa maana nyakati hizi ni za uovu.
17 Kwa sababu hiyo msiwe wajinga, bali mfahamu ni nini yaliyo mapenzi ya Bwana.

Yakobo 3 : 17
17 ⑳ Lakini hekima itokayo juu, kwanza ni safi, tena ni ya amani, ya upole, tayari kusikiliza maneno ya watu, imejaa rehema na matunda mema, haina fitina, haina unafiki.

Mithali 3 : 13 – 18
13 Heri mtu yule aonaye hekima, Na mtu yule apataye ufahamu.
14 ⑪ Maana biashara yake ni bora kuliko biashara ya fedha, Na faida yake ni nyingi kuliko dhahabu safi.
15 ⑫ Yeye ana thamani kuliko marijani, Wala vyote uvitamanivyo havilingani naye.
16 ⑬ Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kulia, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.
17 ⑭ Njia zake ni njia za kupendeza sana, Na mapito yake yote ni amani.
18 ⑮ Yeye ni mti wa uzima kwao wamshikao sana; Ana heri kila mtu anayeshikamana naye.

Mithali 10 : 23
23 Kwa mpumbavu kutenda maovu ni kama mchezo; Bali mtu mwenye ufahamu ana hekima.

Mithali 12 : 15
15 ② Njia ya mpumbavu imenyoka machoni pake mwenyewe; Bali yeye aliye na hekima husikiliza shauri.

Mithali 18 : 15
15 Moyo wa mwenye busara hupata maarifa; Na sikio la mwenye hekima hutafuta maarifa.

Wakolosai 3 : 16
16 Neno la Kristo na likae kwa wingi ndani yenu katika hekima yote, mkifundishana na kuonyana kwa zaburi, na nyimbo, na tenzi za rohoni; huku mkimwimbia Mungu kwa neema mioyoni mwenu.

Mithali 17 : 27 – 28
27 Azuiaye maneno yake ni mwenye maarifa; Na mwenye roho ya utulivu ana busara.
28 Hata mpumbavu akinyamaza, huhesabiwa hekima; Akifumba midomo yake, huhesabiwa ufahamu.

Mhubiri 8 : 1
1 Ni nani aliye kama mwenye hekima; Naye ni nani ajuaye kufasiri neno? Hekima ya mtu humwangaza uso wake, Na ugumu wa uso wake hubadilika.

Yeremia 9 : 24
24 ⑰ bali ajisifuye na ajisifu kwa sababu hii, ya kwamba ananifahamu mimi, na kunijua, ya kuwa mimi ni BWANA, nitendaye wema, na hukumu, na haki, katika nchi; maana mimi napendezwa na mambo hayo, asema BWANA,

Ayubu 12 : 12 – 13
12 Wazee ndio walio na hekima, Na katika kuishi siku nyingi iko fahamu.
13 Hekima na amri zina yeye [Mungu]; Yeye anayo ushauri na fahamu.

Luka 21 : 15
15 kwa sababu mimi nitawapa kinywa na hekima ambayo watesi wenu wote hawataweza kushindana nayo wala kuipinga.

Mithali 19 : 20
20 Sikiliza mashauri, ukapokee mafundisho, Upate kuwa na hekima siku zako za mwisho.

Waefeso 1 : 16 – 19
16 siachi kutoa shukrani kwa ajili yenu; nikiwakumbuka katika sala zangu,
17 Mungu wa Bwana wetu Yesu Kristo, Baba wa utukufu, awape ninyi roho ya hekima na ya ufunuo katika kumjua yeye;
18 macho ya mioyo yenu yatiwe nuru, mjue tumaini la mwito wake jinsi lilivyo; na utajiri wa utukufu wa urithi wake katika watakatifu jinsi ulivyo;
19 na ubora wa ukuu wa uweza wake ndani yetu tuaminio jinsi ulivyo; kwa kadiri ya utendaji wa nguvu za uweza wake;

Mithali 17 : 10
10 Lawama hupenya moyoni mwa mwenye ufahamu, Kuliko mapigo mia moyoni mwa mpumbavu.

Mithali 23 : 12
12 Elekeza moyo wako kusikiliza mafundisho; Tega masikio yako kusikia maneno ya maarifa.

Mithali 14 : 16
16 Mwenye hekima huhadhari, na kujitenga na uovu; Bali mpumbavu hupuuza yote, na hajali.

Mithali 24 : 3 – 7
3 Nyumba hujengwa kwa hekima, Na kwa ufahamu huthibitika,
4 Na kwa maarifa vyumba vyake hujazwa Vitu vyote vya thamani na vya kupendeza.
5 Mtu mwenye hekima ana nguvu; Naam, mtu wa maarifa huongeza uwezo;
6 Maana kwa mashauri ya akili utafanya vita; Na kwa wingi wa washauri huja wokovu.
7 Kwa mpumbavu hekima haipatikani; Hafumbui kinywa chake langoni.

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *