Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia hedhi
Mambo ya Walawi 15 : 19 – 30
19 Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
20 Na kitu chochote ambacho anakalia katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho amekalia kitakuwa najisi.
21 Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
22 Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
23 Kiwe ni katika kitanda, au chochote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hadi jioni.
24 Na mtu yeyote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.
25 Na mwanamke kama akitokwa na damu yake siku nyingi, nayo si katika majira ya kutengwa kwake, au kama anatoka damu kuzidi majira ya kutengwa kwake; siku hizo zote za kutoka damu ya unajisi wake, atakuwa kama alivyokuwa katika siku za kutengwa kwake; yeye ni najisi.
26 Kila kitanda akilaliacho katika siku zote za kutoka damu kitakuwa kama kitanda cha kutengwa kwake; na kila kitu atakachokilalia kitakuwa najisi, kama unajisi wa kutengwa kwake.
27 Na mtu yeyote atakayevigusa vitu vile atakuwa najisi, naye atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
28 Lakini huyo mwanamke akiwa ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
29 Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania.
30 Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
Mambo ya Walawi 20 : 18
18 ⑤ Tena mwanamume akilala na mwanamke aliye na ugonjwa wake, na kufunua utupu wake; amefunua jito la damu yake, naye mwanamke amefunua jito la damu[11] yake; wote wawili watatengwa mbali na watu wao.
Mambo ya Walawi 15 : 19 – 24
19 Mwanamke yeyote aliye na hedhi, atatengwa kwa muda wa siku saba; na mtu yeyote atakayemgusa atakuwa najisi hadi jioni.
20 Na kitu chochote ambacho anakalia katika kutengwa kwake kitakuwa najisi; na kila kitu ambacho amekalia kitakuwa najisi.
21 Mtu yeyote atakayekigusa kitanda chake huyo mwanamke atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
22 Mtu yeyote atakayekigusa chochote ambacho huyo mwanamke amekalia atazifua nguo zake, na kuoga majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
23 Kiwe ni katika kitanda, au chochote alichokikalia huyo mwanamke, atakapokigusa kitu hicho, atakuwa najisi hadi jioni.
24 Na mtu yeyote atakayelala na mwanamke na unajisi ukawa juu yake, atakuwa najisi muda wa siku saba; na kila kitanda alichokilalia kitakuwa najisi.
Ezekieli 36 : 17
17 Mwanadamu, nyumba ya Israeli walipokaa katika nchi yao wenyewe, waliitia uchafu kwa njia yao na kwa matendo yao. Njia yao mbele zangu ilikuwa kama uchafu wa mwanamke wakati wa kutengwa kwake.
Mambo ya Walawi 18 : 19
19 ② Usimwendee mwanamke kufunua utupu wake atakapokuwa najisi kwa ajili ya hedhi.
Mambo ya Walawi 15 : 28 – 30
28 Lakini huyo mwanamke akiwa ametakaswa na kule kutoka damu kwake, ndipo atakapojihesabia siku saba, na baadaye atakuwa safi.
29 Siku ya nane atajipatia hua wawili, au makinda mawili ya njiwa, na kumletea kuhani, mlangoni pa hema ya kukutania.
30 Kuhani atamsongeza mmoja kuwa sadaka ya dhambi, na wa pili kuwa sadaka ya kuteketezwa; naye kuhani atafanya upatanisho kwa ajili yake mbele za BWANA, kwa ajili ya kutoka damu ya unajisi kwake.
Ezekieli 18 : 6
6 hakula juu ya milima, wala hakuviinulia macho vinyago vya nyumba ya Israeli, wala hakumtia unajisi mke wa jirani yake, wala hakumkaribia mwanamke wakati wa kutengwa kwake;
Mambo ya Walawi 15 : 16
16 Na mtu yeyote akitokwa na shahawa yake, ndipo ataoga mwili wake wote majini, naye atakuwa najisi hadi jioni.
Ezekieli 22 : 10
10 Ndani yako wamefunua uchi wa baba zao; ndani yako wamemfanyia nguvu mwanamke asiye safi wakati wa kutengwa kwake.
Mwanzo 31 : 35
35 Naye Raheli akamwambia babaye, Bwana wangu asikasirike kwa sababu siwezi kuinuka mbele yako, maana nimeshikwa na mambo ya kike. Akatafuta, wala hakuviona vile vinyago.
Leave a Reply