Biblia inasema nini kuhusu Hazori – Mistari yote ya Biblia kuhusu Hazori

Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hazori

Yoshua 11 : 1
1 ⑥ Kisha ikawa, hapo huyo Yabini, mfalme wa Hazori, aliposikia habari ya mambo hayo, akatuma mjumbe aende kwa Yobabu, mfalme wa Madoni, na kwa mfalme wa Shimroni, na mfalme wa Akshafu,

Yoshua 11 : 11
11 Nao wakawapiga wote pia waliokuwamo ndani ya Hazori kwa makali ya upanga, wakawaangamiza kabisa; hakubakizwa hata mmoja akiwa hai; kisha akauteketeza Hazori kwa moto.

Yoshua 11 : 13
13 Lakini katika habari ya miji hiyo iliyosimama katika vilima vyao, Israeli hakuteketeza kwa moto miji hiyo, isipokuwa ni mji wa Hazori tu; mji huo Yoshua aliuteketeza kwa moto.

Yoshua 12 : 19
19 mfalme wa Madoni, mmoja; na mfalme wa Hazori, mmoja;

Yoshua 19 : 36
36 Adama, Rama Hazori;

Waamuzi 4 : 2
2 BWANA akawauza na kuwatia katika mkono wa Yabini, mfalme wa Kanaani, aliyetawala huko Hazori; na Sisera, aliyekaa katika Haroshethi wa Mataifa, alikuwa kamanda wa jeshi lake.

Waamuzi 4 : 17
17 Lakini Sisera akakimbia kwa miguu, akaifikia hema ya Yaeli mkewe Heberi, Mkeni; kwa maana palikuwa na amani kati ya Yabini, mfalme wa Hazori, na nyumba ya Heberi, Mkeni.

1 Samweli 12 : 9
9 Lakini wakamsahau BWANA, Mungu wao, naye akawauza na kuwatia katika mikono ya Sisera, jemadari wa jeshi la Hazori, na katika mikono ya Wafilisti, na katika mikono ya mfalme wa Moabu, nao wakapigana nao.

2 Wafalme 15 : 29
29 Katika siku za Peka mfalme wa Israeli akaja Tiglath-pileseri mfalme wa Ashuru, akatwaa Iyoni, na Abel-beth-maaka, na Yanoa, na Kedeshi, na Hazori, na Gileadi, na Galilaya, nchi yote ya Naftali; akawahamisha hao watu mpaka Ashuru.

Nehemia 11 : 33
33 Hazori, Rama, Gitaimu;

Yoshua 15 : 23
23 Kedeshi, Hazori, Ithnani;

1 Wafalme 9 : 15
15 Na hii ndiyo sababu ya shokoa aliyoitoza mfalme Sulemani; ili kuijenga nyumba ya BWANA, na nyumba yake mwenyewe, na Milo, na ukuta wa Yerusalemu, na Hasori, na Megido, na Gezeri.

Nehemia 11 : 33
33 Hazori, Rama, Gitaimu;

Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *