Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hatia
Kutoka 22 : 9
9 ⑮ Kila jambo la kukosana, kama ni la ng’ombe, au la punda, au la kondoo, au la mavazi, au la kitu chochote kilichopotea, ambacho mtu mmoja asema ni chake, hilo jambo la watu wote wawili litaletwa mbele ya Mungu; na yeye atakayehukumiwa na Mungu kuwa ni mkosa atamlipa mwenziwe thamani yake mara mbili.
Kutoka 21 : 36
36 Au ikiwa ilijulikana ya kuwa ng’ombe tangu hapo amezoea kupiga kwa pembe, wala mwenyewe asimzuie; ndipo atakapolipa yeye, ng’ombe kwa ng’ombe, na huyo ng’ombe aliyekufa atakuwa ni wake.
Mathayo 18 : 18
18 ⑦ Amin, nawaambieni, yoyote mtakayoyafunga duniani yatakuwa yamefungwa mbinguni; na yoyote mtakayoyafungua duniani yatakuwa yamefunguliwa mbinguni.
Luka 17 : 4
4 Na kama akikukosea mara saba katika siku moja, na kurudi kwako mara saba, akisema, Nimetubu, msamehe.
Leave a Reply