Hizi ndizo Aya za Biblia zinazozungumzia Hasira
Mwanzo 4 : 6
6 BWANA akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
Mwanzo 49 : 7
7 Ghadhabu yao na ilaaniwe, maana ilikuwa kali, Na hasira yao, maana ilikuwa haina huruma. Nitawagawa katika Yakobo, Nitawatawanya katika Israeli.
2 Mambo ya Nyakati 28 : 9
9 Lakini kulikuwako huko nabii wa BWANA, jina lake aliitwa Odedi; akatoka kuwalaki jeshi waliokuja Samaria, akawaambia, Angalieni, kwa kuwa BWANA, Mungu wa baba zenu, aliwakasirikia Yuda, yeye amewatia mikononi mwenu, nanyi mmewaua kwa ghadhabu iliyofikia mbinguni.
Ayubu 5 : 2
2 Kwani hasira humwua mtu mpumbavu, Nao wivu humwua mjinga.
Ayubu 19 : 29
29 Uogopeni upanga; Kwa maana adhabu za upanga zina ghadhabu, Mpate kujua ya kwamba hukumu iko.
Zaburi 37 : 8
8 Ukomeshe hasira, uache ghadhabu, Usikasirike, mwisho wake ni kutenda mabaya.
Zaburi 55 : 3
3 Kwa sababu ya sauti ya adui, Kwa sababu ya dhuluma yake yule mwovu. Kwa maana wananitupia uovu, Na kwa ghadhabu wananiudhi.
Zaburi 76 : 10
10 ⑪ Maana hasira ya binadamu itakusifu, Masalio ya hasira utajifunga kama mshipi.
Mithali 6 : 34
34 Maana wivu ni ghadhabu ya mtu; Wala hatahurumia siku ya kujilipizia kisasi.
Mithali 12 : 16
16 Ghadhabu ya mpumbavu hujulikana mara; Bali mtu mwerevu husitiri aibu.
Mithali 14 : 17
17 Yeye aonaye hasira upesi atatenda kwa ujinga; Na mtu mwenye hila mbaya huzirwa.
Mithali 14 : 29
29 Asiye mwepesi wa hasira ana fahamu nyingi; Bali mwenye roho ya hamaki hutukuza upumbavu.
Mithali 15 : 1
1 Jawabu la upole hugeuza hasira; Bali neno liumizalo huchochea ghadhabu.
Mithali 15 : 18
18 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Bali asiye mwepesi wa hasira hutuliza mashindano.
Mithali 16 : 14
14 Hasira ya mfalme ni kama wajumbe wa mauti; Lakini mtu mwenye hekima ataituliza.
Mithali 16 : 29
29 Mtu mkali humshawishi mwenzake; Humwongoza katika njia isiyo njema.
Mithali 16 : 32
32 Asiye mwepesi wa hasira ni mwema kuliko shujaa; Na mtu aitawalaye roho yake kuliko mtu atekaye mji.
Mithali 17 : 14
14 Mwanzo wa ugomvi ni kama kutoboa penye maji; Basi acheni ugomvi kabla haujafurika.
Mithali 19 : 12
12 Ghadhabu ya mfalme ni kama ngurumo ya simba; Bali hisani yake kama umande juu ya majani.
Mithali 19 : 19
19 Mtu wa hasira nyingi atachukua adhabu yake, Maana ujapomwokoa huna budi kufanya tena.
Mithali 21 : 24
24 Mwenye kiburi na kutakabari, jina lake ni mbishi; Hutenda mambo katika majivuno ya kiburi chake.
Mithali 22 : 25
25 Usije ukajifunza njia zake; Na kujipatia nafsi yako mtego.
Mithali 25 : 28
28 Asiyetawala roho yake Ni mfano wa mji uliobomolewa, usio na kuta.
Mithali 27 : 4
4 Ghadhabu ni kali, na hasira ni gharika; Lakini ni nani awezaye kusimama mbele ya wivu.
Mithali 29 : 9
9 Mwenye hekima akijadiliana na mpumbavu; Akikasirika au akicheka, pia hapana raha.
Mithali 29 : 22
22 Mtu wa hasira huchochea ugomvi; Na mtu mwenye ghadhabu huasi sana.
Mithali 30 : 33
33 Kwa maana kupiga maziwa huleta siagi; Na kupiga pua hutokeza damu; kadhalika kuchochea hasira hutokeza ugomvi.
Leave a Reply